Mfanyakazi wa uwanja wa Ndege wa Bukoba Bi Leiner Rogatus akifurahi mara baada ya kununua simu Huawei 330 kwa sh 130,000 Nje ya uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambao kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo ilikuwa ikitambulisha huduma zake mbalimbali kwenye kampeni ya Tigo welcome pack mwishoni mwa wiki
Meneja bidhaa wa Tigo Bw.Robert Paul akiongea na wafanyabiashara wa soko la Kaisho wilayani Karagwe kuhusu Tigo Kilimo hii ni moja ya kampeni za Tigo welcome pack zinazoendelea mikoa mbalimbali nchini.
Msanii wa bongo fleva Sunday Mjeda maarufu Linex akitoa burudani kwenye tamasha la Tigo welcome pack lililofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kampeni ya welcome pack inawawezesha wateja wa Tigo kujua huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni ya Tigo.
Wasanii wa kundi la Original Komedi wakitoa burudani kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati wa kampeni ya kifurushi cha Tigo welcome pack, Kifurushi hicho kitamwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakika 20, mb175,sms bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo
Wasanii Emmanuel Mgaya Maarufu Masanja Mkandamizaji na Slivery Mujuni maarufu Mpoki wakitoa burudani kwa wakazi wa Bukoba waliofurika kwenye uwanja wa Kaitaba wakati wa onesho la Tigo welcome pack
No comments:
Post a Comment