Sunday, November 9, 2014

TAARIFA RASMI YA UPASUAJI ALIOFANYIWA RAIS KIKWETE

Jana asubuhi tarehe 8 Novemba Mheshimiwa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa Tezi Dume katika Hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore Maryland nchini Marekani upasuaji ambao ulimalizika salama. Leo tarehe 9 Novemba ni siku ya pili baada ya upasuaji na Mheshimiwa Rais anaendelea vizuri. Mapema asubuhi ya leo alianza mazoezi ya kutembea. Tutaendelea kuwashirikisha taarifa za maendeleo ya Mheshimiwa Rais 
Post a Comment