Saturday, December 20, 2014

HAYA NDIO MAENEO YA MIJI AMBAYO CHADEMA IMESHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA






DK slaa Akiyataja maeneo ya Miji midogo ambayo CHADEMA imeshinda, Dr. Slaa amesema
"1. Nkasi - Namanyere
2. Hai - Bomang'ombe.
3.Karatu - Karatu.
4. Arumeru Mashariki - Usa river.
5.Vunjo - Ukawa.
6. Mbeya vijijini - Mbalizi.
7. Mbozi Maghari - Tunduma.
8. Mbozi Mashariki - Mlowo.
9. Kyela - Kyela.
10. Lupa - Makongorosi.
11. Busanda - Katoro.
12. Geita - Geita.
13. Chato - Chato.
14. Kwimba - Ngudu.
15. Karagwe - Kayanga.
16. Bukombe - Ushirombo.
17. Sengerema - Sengerema.
18. Tarime - Tarime.
19. Tarime - Sirari mji mdogo.
20. Rorya - Shirati ( 7/2).
21. Bunda - Bunda.
22. Serengeti - Mugumu 10/10 ( CUF 3).
23. Kahama - Kahama.
24. Bariadi - Bariadi ( 49/43).
25. Kilombero - Ifakara.
26. Magu - Magu.
27. Mbozi - Vwawa.


HAPA CHINI NI TAARIFA YA MAAZIMIO CHADEMA(Katika Mkutano Mkuu wa Tano wa chama)

 

Baadhi ya maazimio ya CHADEMA kuhusu uchaguzi serikali za mitaa kama yalivyosomwa na Dr. Slaa (Pichani) alipozungumza na waandishi wa Habari.
¤ Suala la kupita bila kupingwa ni kinyume na Demokrasia na haki ya msingi ya raia ya kuchagua, hivyo utamaduni huu ufe nakama ikitokea basi zipigwe KURA za NDIO na HAPANA.
¤ Viongozi wa CHADEMA waliochaguliwa ikigokea wanatuhumiwa kwa vitendo vya rushwa kamwe chama hakitawavumilia viongozi hao na tutawachukulia hatua maramoja bila kusita ikiwemo za ndani ya chama na hata kuwashtaki mahakamani.
¤ Kamati kuu imezitaka mamlaka zinazohusika kuwatambua mabalozi wa CHADEMA katika masuala yote ambayo yanahitaji wa ngazi hiyo, ikiwemo utambulisho wa ukazi. Wanachama wa CHADEMA hawalazimiki kwenda kupata idhini ya mabalozi wanaotokana na CCM kama ambavyo serikali inataka.

KUHUSU MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2015.

Kamati Kuu ya Chama imepokea kwa masikitiko taarifa zinazoonesha kuwa hadi sasa serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi haionekani kujipanga kuweza kufanikisha uchaguzi mkuu ujao.
Tayari kasoro nyingi ambazo kama hazitafanyiwa kazi zitasababisha vurugu huko tuendako zimeanza kuonekana kwenye zoezi la majaribio ya uandikishaji wapiga kura linaloendelea hadi sasa Kawe,Kilombero, na Mlele.
Akizungumzia vurugu na vifo na kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi huo, Dr. Slaa amewalaumu Waziri mkuu Mh. Pinda na Waziri wa TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia kuwa ndio chanzo cha matukio yote katika uchaguzi huo. Hasa kwa kutunga kwao kanuni mbovu na miongozo katika sheria ya uchaguzi Serikali za mitaa kanuni ambazo zimepelekea mauji katika baadhi ya maeneo nchoni hasa kule Nzega kutokea. Hivyo wote hawa wanapaswa kujiuzulu wenyewe ama wawajibishwe na Mh. Raisi mara moja.

No comments: