Wednesday, December 24, 2014

HOTUBA YA JK YAWAIBUA UKAWA UPYAAA,SOMA WALICHOSEMA KUHUSU SAKATA LA ESCROW LEO

Viongozi wakuu wa ukawa wakingozwa na mwenyekiti wa CUF IBRAHIMU LIPUMBA,mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI JAMES MBATIA,pamoja na katibu mkuu wa chadema DK WILBROD SLAA wakiwasili katika ukumbi wa mkutano na wanahabari leo makao makuu ya CUF buguruni jijini Dar es salaam
Ikiwa ni siku kadhaa baada ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dk JAKAYA KIKWETE kuzungumza na taifa kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha za account ya TEGETA ESCROW.Nao umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wameibuka na kumvaa rais kwa kile walichokiita ni hotuba ya kulifedhehesha taifa kwani imeonyesha wazi kuwatetea wahusika wakuu wa sakata hilo.

Wakizungumza na wanahabari muda huu jijini Dare s salaam mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambaye ni mwenyekiti wa CUF profesa IBRAHIM LIPUMBA amesema kuwa hotuba ya rais kikwete ni hotuba mbovu na imelenga wazi wazi kuuficha ukweli wa sakata hilo kwa kuwatetea wahusika hao huku akisema umoja wao hautachoka kulipigania swala hilo hadi mwisho.

Profesa lipumba anasema kuwa ni jambo la ajabu kuona kuwa rais anashindwa kuwachukulia hatua kali wahusika kama mmiliki wa PAP singasinga HARBINDER SINGH pamoja na james rugemarila ambao kwenye kamati na report zote wanatajwa kuwa wao ndio waliohusika katika mchakato huo wa uchakataji wa pesa hizo
Profesa LIPUMBA akizungumza na wanahabari
“hivi huyu singasinga ana nini,amempa nini rais,yani ameiweka serikali mkonono au mfukoni,maana rais hataki hata kumgusa,ni jambo la kustajaabisha sana kuona rais anawanyamazia wawekezaji wezi kama huyu ambao wanawaibia watanzania mchana kweupe”alihoji lipumba

Aidha amesema kuwa ni lazima rais ajue kuwa kazi yake sasa ni kutekeleza maamuzi ya bunge ambayo yalipitishwa na wabunge wote kwa umoja wao na waziri mkuu akiwemo na sio kuanza kufanya uchunguzi upya kwani uchunguzi ulishafanyika kinachotakiwa sasa ni utekelezaji tu.
Katibu mkuu wa chadema dk SLAA akizngumza ambapo amesema kuwa taifa limefika mahali ambapo sio huku akisema kuwa idara ya usalama wa taifa imelala na inashirikiana na wezi kwani sakata la escrow walikuwa wanaliona na wakalifumbia macho kana kwamba hawalioni na badala yake wanaenda kulinda mikutano ya kisiasa ya wapinzani badala ya kuwakamata wezi wa mabilioni ya watanzania.
UKAWA wamesema kuwa pamoja na hotuba aliyoitoa rais pamoja na kuwawajibisha watu kadhaa bado haitoshi kwani bado kuna watu wengi ambao wamehusika na sakata hilo na liko wazi hivyo wafikishwe mahakamani mara moja kwa ubadhilifu wa mali ya umma.

“Tunataka yafuatayo yafanyike, kwanza kikao kijacho cha bunge kiwawajibishe serikali kwa kushindwa kutekeleza maazimio yao.ukawa tutaendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu sakata hilo,hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote waliohusika,pia sheria ya maadili itungwe upya iweke wazi mali za viongozi wetu wa umma”ameongeza lipumba.
James mbatia akizungumza kwa uchungu amesema kuwa Tanzania sasa hali ni mbaya kutokana na wizi huo ambapo amesema kuwa wafanyakazi mbalimbali ukianza na wabunge hawajalipwa fedha zao kutokana na kukosekana kwa hela huku serikali ikiendelea kunyamaza kimya kwa wizi mkubwa kama huu kuwahi kutokea nchini Tanzania
Katika hatua nyingine UKAWA wametangaza kuitisha maadamano na mikutano nchi nzima kama serikali itaendelea kuwatetea wezi wa fedha hizo za watanzania,kulenga kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu ukweli wa sakata hilo na hatua ambazo zinachukuliwa na serikali kwa sasa

No comments: