Wednesday, December 31, 2014

HUYU NDIYE KOCHA MPYA WA SIMBA,ASAIN MWAKA MMOJA

GORAN AMWAGA WINO KWA MWAKA MMOJA KUINOA SIMBA

KOCHA mpya wa Simba raia wa Serbua Goran Kopunovic amemwaga wino wa mwaka
mmoja kuinoa timu hiyo ya Msimbazi.


Mmoja wa viongozi wa Simba aliiambia blog ya jamii kuwa kocha huyo aliyewasili leo
asubuhi na kufikia kwenye hotel ya Double Tree Masaki ataondoka kesho kwenda
Zanzibar kujiunga na timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi inayoshiriki michuano ya Kombe
la Mapinduzi.


Naye Kopunovic akizungumza muda mfupi baada ya kukanyaga hardhi ya Tanzania 
alisema "Nimekuja kufanya kazi, naamini nitapata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa 
Simba, wachezaji na mashabiki, Simba ni timu kubwa, naamini nitawapa 
mafanikio."alisema

Kocha huyo, amechukua mikoba ya Patrick Phiri aliyefungashiwa virago baada ya uongozi 
wa Simba chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva kufanya tathmini ya mwenendo wa timu 
ambapo ametoka sare mechi sita, ameshinda mechi moja na kupoteza moja hivyo kuona 
hastaili kuendelea kuinoa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi huku akidaiwa kukaidi agizo la 
viongozi la kutowachezesha Waganda katika mechi dhidi ya Kagera walionyukwa bao 1-0

No comments: