Wednesday, December 10, 2014

TIGO YATOA DOLA 40,000 KWA MIRADI YA WAJASIRILIAMALI JAMII

unnamedMkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akimkabidhi cheti cha ushiriki kwenye shindano la Tigo Digital Changemakers kwa Severin Philemon wakati wa kutangaza washindi wa shindano hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
unnamed1Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akimkabidhi cheti cha ushiriki kwenye shindano la Tigo Digital Changemakers kwa Mohamed Juma wakati wa kutangaza washindi wa shindano hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez (kushoto) akiwa na mmoja wa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers, Leka Tingitana, mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa hundi wa dola 20,000 za Kimarekani ikiwemo cheti cha ushiriki kutoka Tigo na Reach for Change mapema leokwa mradi wake wa kijitali eAfya.
unnamed3Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez (kushoto) akiwa na mshindi mmoja wa shindano la Tigo Digital Changemakers Innocent James Sulle mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa hundi dola 20,000 za Kimarekani ikiwemo cheti cha ushiriki kutoka Tigo na Reach for Change mapema leo kwa mradi wake wa kijitali Travelling Library.
unnamed6 Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa Reach For Change Bi.Amma Lartey(kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano la Tigo Digital Changemakers, Leka Tingitana na Innocent James Sulle baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lenye kutumia nyenzo za kidijitali kwa ajili yakuwasaidia watoto nchini.
……………………………………………………………………………..

Tigo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali Reach for Change leo imetangaza washindi wawili wengine wa wajasiriliamali jamii watakaodhaminiwa kiasi cha dola elfu 20,000 kila mmoja kwa ajili ya kuendesha miradi yao inayolenga kuinua hali ya maisha ya watoto nchini. 
Washindi hao walichaguliwa katikati ya ushindani mkali ambapo mamia ya maombi na mawazo zaidi ya 557 yenye kutumia nyenzo za kidijitali kwa ajili yakuwasaidia watoto nchini yalipokelewa, alisema Mkurugenzi Mkuu Diego Gutierrez katika tafriija maalum jijini Dar es Salaam.
Majina na miradi ya wawili hao ambao wanaungana na washindi wengine watano wa nyuma kama wajasiriliamali jamii katika shindano la Tigo Digital Changemakers ni kama ifuatayo:
1. Leka Tingitana, eAfya;
o Hii ni teknolojia inayotumika kuongeza ufanisi katika mawasiliano na utendaji wa kazi wa sekta ya afya nchini kwa kuwafikishia huduma za afya wagonjwa kwa uharaka zaidi. Teknolojia hii inawalenga watumishi wa afya katika jamii. 
2. Innocent James Sulle, Travelling Library;
o Hii ni maktaba maalum ya kidijitali kwa ajili ya kuwapatia watoto fursa ya kujenga tabia ya kusoma vitabu kupitia njia za kusoma kielektroniki. 
“Tunayofuraha kubwa sana kufanikisha miradi ya kibunifu yenye suluhu za kidijitali kuweza kuinua hali ya maisha ya watoto nchini. Hii inadhihirisha kwamba tunadhamira ya dhati kabisa ya kusaidia jamii kupitia suluhu za kidijitali na hasa hasa katika kuwekeza kwa watoto ambao ndio taifa la kesho,” alisema Gutierrez.
Aliendelea, “Wajasiriliamali hawa wawili wataingia katika mpango maalum wa maendeleo ambapo watapatiwa msaada wa kubadilisha mawazo yao kuwa miradi endelevu. Mbali na dola 20,000 wanazo zawadiwa, pia watapatiwa uongozaji maalum na ushauri wakitaalam kutoka maafisa waandamizi wa Tigo na Reach for Change.” 
Agosti mwaka huu, Tigo na Reach for Change walizindua kwa mara ya tatu nchini Tanzania mpango huu wenye malengo ya kuwatafuta na kuwasaidia wajasiriliamali jamii wenye mawazo mazuri ya kidijitali ya jinsi ya kusaidia kuinua hali ya maisha ya watoto.
Mkurugenzi wa Kanda wa Reach for Change nchini Tanzania Amma Lartey pia aliwapongeza washindi hao pamoja na washiriki wote wa shindano la Tigo Digital Changemakers kwa kile alichoita “miradi mizuri” ambayo yalijaa ubunifu mkubwa.
Hakika ilikuwa mchakato wenye ushindani mkubwa kuweza kuwachagua washindi wawili tu kati ya mamia na mamia ya miradi ambayo tulipokea. Imechukua zaidi ya miezi mitatu kuweza kupitia na kuchuja maombi ya kila mmoja aliyetuma na kuweza kufanya usaili kwa baadhi ya wale waliopita katika mchujo. Tunayofuraha kwamba mchakato huu umeisha kwa mafanikio makubwa huku tukiwapata washindi hawa wawili ambao tunaamini miradi yao yatakuwa chachu kubwa katika kuchangia kuleta maisha bora kwa watoto wengi nchi nzima,” Lartey alisema. 
Tigo na Reach for Change ilianza mchakato wa kuwatafuta wajasiriliamali jamii kutoka kila nchi ambayo kampuni ya Tigo inafanya kazi barani Afrika kuanzia Agosti 2012, mashindano hayo yalianzia Rwanda, ikifuatiwa na Tanzania, Congo DRC, Ghana, Chad halafu Senegal.
Mpango huu wa Digital Changemakers ipo katika malengo ya Tigo ya kuleta maisha ya kidijitali nchini. Huu ni mwaka wa tatu tangu Tigo na Reach for Change wameanza kwa pamoja kuwadhamini wajasiriliamali jamii kuweza kutimiza miradi yao. Kwa muda huo wajasiriliamali jamii watano wamekwishapatiwa msaada wa kifedha kwa ajili ya kuendesha miradi yao ambapo mpaka sasa watoto 9,500 wameshanufaika nchi nzima

No comments: