Thursday, December 11, 2014

WLAC WAZINDUA REPORT YAKE YA WATOTO WALIOPO MAGEREZANI,TUKIO NZIMA NA KILICHOZUNGUMZWA KIPO HAPA

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria MAIMUNA TARISHI pamoja na kaimu  mkurugenzi wa WLAC wakizundua report hiyo mapema leo 

Chama cha wanawake wanasheria Tanzania WLAC leo kimezindua report yake ya hali ya watoto waliopo katika magereza kwa makosa mbalimbali ya jinai report ambayo inaonyesha bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakuta watoto wanaotumikia adhabu mbalimbali katika magereza huku wadau wakiombwa kuwatafitia ufumbuzi watoto hao kwani bado ni msaada kwa taifa.


Akisoma mambo kadhaa yanayopatikana katika report hiyo mwanasheria mkuu wa WLAC ROBERT CHUWA amesema kuwa moja ya changamoto kubwainayowakumba watoto wanaotumikia adhabu katika magereza yetu ni pamoja na kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu makosa waliyofanya pamoja na kukosa watu wa kuwapa elimu hiyo kwa muda muafaka.

Aidha amesema kuwa chanagamito nyingine iliyopo katika mahakama zetu pamoja na polisi watoto kudanganya umri wao pindi wanapokutwa na makosa kwa lengo la kuepuka adhabu za watu wazima na kudanganya kuwa wana umri chini ya miaka 18.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa katibu mkuu wizara ya katiba na sheria mh MAIMUNA TARISHI pamoja na kuwapongeza WLAC pamoja na wadau wengine kwa kutoa msaada wa kisheria kwa watoto waliopo magerezani amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wanaendelea kuwasaidia watoto hao kwa hali na mali kwani wanatambua fika kuwa watoto hao wanahitaji msaada wa kisheria ili kubadilika na kuwa katika hali nzuri

mwanasheria mkuu wa WLAC ROBERT CHUWA ambaye ndiye moja ya watu walioandaa report hiyo akitoa machache yaliyopo ndani ya report hiyo

Awali akizungumza kaim mkurugenzi wa WLAC BI GRACE DAFA amesema kuwa hapo awali walikuwa hawatoi msaada wa kisheria kwa makosa yanayowahusu watoto lakini ilipofika mwaka 2000 kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakaanza kutoa msaada huo wa kisheria kwa kutumia sharia ya mwaka 2009 ya watoto ambayo ilitaka watoto wenye makosa wahukumiwe kama watoto na sio watu wazima na ndipo shirika hilo lilianza rasmi kuwatetea watoto.

Shirika la WLAC lilianza rasmi kufanya kazi zake mnamo mwaka 1989 nchini Tanzania na hadi sasa limekuwa na mafanikio makubwa kwa kutoa msaada wa kisheria katika Nyanja mbalimbali
VICTORIA MGONELA ambaye ni mtaalam wa ulinzi na usalama wa mtoto UNICEF ambao wao ndio wadau wakubwa wa WLAC waliofanikisha kupatikana kwa report hiyo akizungumza katika hafla hiyo


Wadau mbalimbali waliohudururia katika uzinduzi huo



Kaimu Mkurugenzi wa WLAC BI GRACE DAFA akizungumza katika hafla hiyo.

No comments: