Thursday, January 29, 2015

BINTI WA MIAKA 22 ASHINDA MILIONI 100 ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544

Mkazi wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magendenye (22) , leo ameibuka mshindi wa kwanza wa  shilingi milioni 100  katika droo ya kumi na nne ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Magedenge binti mwenye umri wa miaka  22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika  nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo   amesema kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa  kazini   na amefurahia ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Katika maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha biashara ya  maduka ya M-Pesa pia kufungua  nyumba yangu ya kulala wageni na kusaidia   ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha”.Alisema

“.Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza sala zangu .
Aliongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka  wateja wote kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-
Naye  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania  alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2  wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja  na  maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha  kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.

No comments: