Thursday, January 29, 2015

LHRC NAO WATOA KAULI KUHUSU SAKATA LA KUPIGWA KWA LIPUMBA,SOMA HAPA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu  Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizngumza na wahabari mapema leo
Sakata la kupigwa na kudhalilishwa kwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa IBRAHIMU LIPUMBA katika maandamano ya chama hicho juzi huko Temeke limeendelea kulaaniwa kila kona ambapo leo kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC wameibuka na kauli ya kulaani kitendo hicho na kusema ni kitendo cha kinyama na kinachoididimiza democrasia ya Tanzania.
            
 Akizungumza na wanahabari katika mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili mapungufu ya katiba pendekezwa na sheria ya kura ya maoni Mkurugeni mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria na katiba ya Tanzania na maandamano ni haki ya kila mtanzania hivyo kitendo kinachofanywa na polisi kujaribu kuwanyamazisha watanzania kwa kuzuia maandamano ambayo ni ya amani ni kitendo kibaya na kisipopigwa marufuku kitalipekeka taifa la Tanzania mahali ambapo sio pazuri.

Mwanasheria kutoka LHRC  HAROLD SUNGUSIA akizungumza katika mkutano huo ambao unafanyika katika ukumbi wa ubungo plaza jijini DAR ES SALAAM
  Katika mdahalo huo ambao umehudhuriwa na baadhi ya wanahaharakati wa kuitafuta katiba akiwemo aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba HAMFREY POLEPOLE na   wadau wengine wameendelea kupinga kwa kasi mchakato wa kupata katiba kuendelea kwa kile ambacho wanadai ni kukosa uhalali wa kisiasa na mapungufu mengi ambayo yapo katika sheria ya kura ya maoni ambayo itasimamia mchakato huo
Aliyekuwa mjumbe wa tume ya jaji WARIOBA kijana HAMFREY POLE POLE akizungumza na wanahabari kuhusu mapungufu yaliyopo katika katiba iliyopendekezwa na kasoro nyiungi zilizopo katika mchakato mzima wa kupata katiba mpya
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo


No comments: