Friday, January 23, 2015

HABARI NZITO--LHRC NAO WATAKA KURA YA KATIBA PENDEKEZWA KUAHIRISHWA,SOMA SABABU ZAO HAPA


Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki zabinadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya mchakato wa kura ya maoni juu ya katiba pendelezwa
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC leo kimeungana na baadhi ya wanahabarakati wanaotaka mchakato wa kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa kuahirishwa mpaka hapo daftari la wapiga kura litakapokuwa tayari ikiwa ni pamoja na mapungufu mengine yanayojitokeza katika mchakato huo kurekebishwa.

Akizungumza na wanahabarari asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikifwatilia mchakato huo kwa karibu ikiwa ni pamoja na kusoma sheria ya kura ya maoni ambapo wamebaini mapungufu mengi na endepo yasipofanyiwa marekebisho yanaweza kuathiri zoezi zima la kura ya maoni na kuwanyima haki watanzania wengi kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa Tanzania.

Akitaja mapungufu makubwa ambayo yanaukumba mchakato huo Bi HELLEN amesema changamoto ya muda bado ni kubwa ambapo kwa mujibu wa sheria ya kura ya maoni Tume ya Taifa ya uchaguzi inapaswa kuboresha daftari la wapiga kura ndipo ipigwe lakini hadi leo terehe 23 mwezi huu hadi 28 february ni siku 36 tu na haionyeshi kuwa kuna muda wa kutosha wa kuboresha daftari la kudumu pamoja na vitambulisho vipya.

Aidha ameyataja meneo mengine ambayo yana matatizo kuelekea kura hiyo ni uteuzi wa kura ya maoni ,vituo vya kupigia kura ambapo sheria inaelekeza kuwa tume inaweza kutotumia majimbo ya kawaida na kutengeneza majimbo mapya ambapo amesema kuwa inaweza kuwa hatari kwani tume inaweza kuvuruga zoezi nzima kwa kutotenga vituo sahihi kulingana na uuwiano wa watu
Wanahabari wakiwa makini kusikiliza sakata hilo

Maeneo mengine yenye kasoro ni usajili wa kamati za kura za maoni,utangazaji wa matokeo ya kura ya maoni,pingamizi la matokeo,kulipia gharama ya shauri,upigaji kura kwa walio nje ya kituo,pamoja na swala la rufaa.

Katika hatua nyingine LHRCwameshauri kuwa sheria ya kura ya maoni ipelekwe tena bungeni ifanyiwe marekebisho hayo ya msingi,pamoja na serikali kutoa nakala za kutosha za katiba pendekezwa kwa wananchi waweze kuendelea kuielewa wakati maswala mengine yanaendelea kufanyiwa kazi.
 UKITAKA KUSOMA TAMKO LAO BONYEZA CHINI HAPO MDAU






No comments: