Wednesday, January 21, 2015

HII NDIO TAARIFA YA SIMANZI TULIYOAMKA NAYO ASUBUHI WATANZANIA



Taarifailiyoenea asubuhi ya leo ,inaeleza kuwa majambazi yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar  aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.

 Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika Tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani

Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabom ya machozi na risasi 60 za smg. 

tutaendelea kujuzana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

No comments: