.

HOJA YA KUWAPIMA AFYA WAGOMBEA URAIS YAANZA KUSHIKIWA BANGO,JUKATA NAO WASEMA YAO

Mwenyekiti wa jukwaa la kitiba nchini (JUKATA) Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi leo
NA KAROLI VINSENT


  HUKU zikiwa zimebaki miezi michache tu,kabla ya kipenge akijapulizwa ili kuashiria Kampeni za Uchaguzi wa Mwaka 2015 kuanza,Nao Jukwaa La Katiba nchini JUKATA,limeibuka na kusema Serikali iwapime afya wagombea wa urais kabla ya hawajaenda kwa wananchi ili kuliokoa Taifa  lisiingie kwenye matatizo ya kufa marais  kama yalioikumba nchi Jirani ya Zambia,Ambao wao waliitisha uchaguzi Mkuu baada ya kufariki Michael Chilufya Satta
   
            Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa jukwaa la kitiba nchini (JUKATA) Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambao uliitishwa mahususi kuzungumzia hali ya uchaguzi uliomalizika nchini Zambia ambapo Jukwaa hilo la Katiba liliwakilisha  mwavuli wa asasi za kiraia 184,waliokuwa nchini Zambia wakiangalia mwenendo wa uchaguzi huo,ambapo pamoja na Mambo mengine Kibamba-
           Alisema kuna haja ya watu wanaojitokeza katika nafasi ya kuwania Urais wakapimwa afya zao mapema kabla hawajaruhusiwa kugombea nafasi ya Urais.


          “Tumeshudia mambo ya nchini Zambia katika vipindi vya miaka miaka nane wamekufa marais wawili na kuifanya Zambia iitishe uchaguzi mara kwa mara,na tunaitaka serikali nchini iige walichokifanya Zambia kabla hawajawaruhusu wagombe wa uchaguzi ulimalizika”
    
           “ Na kuwataka wapime afya,maana hata nyumbani tumewaona wagombea wengi hususani hawa wanaoutaka urais kwa udi na uvumba halafu Afya zao ni mbovu maana wamekuwa wagonjwa na hata kama hawa tukiwaacha watafia ikulu na kuitia nchini Hasara kubwa”alisema Kibamba.
        

           Kibamba aliongeza kuwa sababu kubwa ilioifanya nchi ya Zambia kushuka shiringi yao imetokana na kufanya uchaguzi mara kwa mara kwa ngazi ya urais na akasema hii inatakiwa kuwa fundisho kwa nchi kama Tanzania ambao imekuwa na watu wengi wakiutaka nafasi ya urais kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015.

      
          Kauli hiyo ya Kibamba imekuja miezi michache kupita baada ya Mwenyekiti Mkoa wa Mwanza Anthony Diallo kumtuhumu Waziri aliyejiuzulu Edward Lowassa,ambaye nae ni miongoni mwa watu wanaouta Urais kwa udi na Uvumba hapo mwezi wa kumi , ambapo Diallo alisema Lowassa ni mgonjwa na afya yake ni mbaya na kuitahadhirisha chama cha mapinduzi kuwa makini wakati wakuwapitosha wagombe.
       
          Katika hatua nyingine Jukwaa hilo la Katiba nchini JUKUTA limeungana Umoja wa vyama vikuu vya upinzani vinavyounda UKAWA kupinga na  kura ya Maoni ya kupitisha Katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la Katiba inayotarajiwa kufanyika mweshoni mwa mwezi wa nne mwaka huu na kusema hiyo itakuwani ndoto.
      
             Kauli ya Jukata ilitolewa kwa kupitia mwenyekiti wao na kusema Rais Kikwete anadanganywa na wasaidizi wake wanaofosi kufanyika kura ya maoni huku daftari ka kupiga kura likiwa limeshindikana.
       
             Aidha,Kibamba alisema hata Katiba yenyewe iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba bado haijafika hata kwenye asasi zao kiraia ili waweze kutoa elimu kwa wananchi

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.