Tuesday, January 27, 2015

TIZAMA VIJANA WA CHADEMA WALICHOKIFANYA HUKO MUFINDI KASKAZINI

WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa ali
yekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
 Makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kasikazini
WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwahutubia wananchi wa jimbo la mufindi kusini ambako anatarajia kugombea ubunge kupitia Chadema.
  ……………………………………………………………………………………………
Wananchi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamelalamikia ugumu wa maisha
wanaokumbana nao kila kukicha licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa
rasilimali ya misitu pamoja na mazao ya biashara

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wilayani mufind Williamu Mungai mmoja wa wananchi hao Clement Mwachanga alisema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya inayofanya vema kwa kuingiza
pato kubwa la taifa lakini wananchi wake wako katika wimbi kubwa la umaskini
Mwachanga amesema anashangaa wilaya kama ya mufindi inayoongoza kwa utoaji wa mbao nyingi lakini cha kushangaza shule nyingi za msingi hazina madawati jambo linalopelekea wanafunzi wengi kukaa chini.
‘’Hii ni aibu kubwa sana kwa wilaya yetu haiwezekani wilaya inarasilimali za kutosha
lakini wananchi wake wengine wanashidwa hata kupata mlo mmoja kwa siku huku
watoto wao wakishidwa kupelekwa shule kutokana na kushidwa kulipa ada ya kumuandikishia mtoto ”
Kwa upande wake Williamu Mungai ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kulichukua
jimbo hilo la mufindi kaskazi ambalo kwa sasa linaongozwa na naibu waziri wa
maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa amewataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha
watoto wote wanaandikishwa shule za msinga hata kama hawana ada ya
kuandikishiwa kwa kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania
Mungai alisema ni kila mtoto ana haki ya kupata elimu ya msingi kwa kuwa ndivyo katiba
inavyosema na kuwataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarudisha
majumba watoto kwa kisingizio cha kukosa hela ya kuwaandikishia
“Niwatake wenyeviti wangu wa mitaa muhakikishe watoto wote wanaandikiswa na kama
kuna mwalimu atagona kumuandikisha kwa kisingizio eti hana shilingi eflu
hamsini jikusanyeni pamoja niiteni na mimi twende wote tuone kama hata
muandikisha kwa maana walishasema elimu bure sasa bure waliyosema ikuwapi”
alisema Mungai
Hata hivyo mungai alisema imefika wakati wakuikomboa mufindi iliyoko katika wimbi la
umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuataka wanamufindi
kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maono ya mbali katika kuwalete
maendeleo na sio porojo za kila siku. 
Mungai alisema kuwa atahakikisha anazunguka vijiji vyote 72 vya wilaya ya
mufindi katika harakati zake za kujenga chama na kuweza kutambua kero za
wananchi na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua .

No comments: