.

KITUKO--SAMSONI MWIGAMBA APIGWA NA WANACHAMA HADHARANI

Pichani Aliyekwidwa ni katibu mkuu wa Muda wa chama cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba jana 

NA KAROLI VINSENT

SAMSON Mwigamba aliyefukuzwa ndani ya chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema kutokana na kuandaa mipango ya kutaka kuupindua uongozi wa Chadema,na kukimbilia kwenye chama kipya cha Siasa cha ACT-Tanzania na pia huko kaandaa mgogoro mzito na viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Kadawi limbu ambapo sasa wamefukuzwa.
      
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida jana katika  ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ambapo Samson Mwigamba kuchezea  kichapo kutoka kwa   makundi yanayopingana ndani ya Chama cha ACT-Tanzania, tukio hilo lilimkuta wakati Mwigamba alipotoka kwenye kikao cha Usuluhishi wa makundi hayo
Mwigamba ambaye pia ni Katibu Mkuu wa mda ndani ya ACT-Tanzania inadaiwa ghafla walitokea vijana wanaodaiwa kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbu na kumvamia
         Vurugu hizo zimetokea ikiwa ni siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kumsimamisha uongozi Limbu na kumwondoa katika nafasi yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa makosa ya kinidhamu.
        
Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu wanasema sababu ya Mwigamba kuvamiwa inatokana na kumtapeli kiongozi mwezake wa Chama hicho mkoani Arusha milioni moja .
Bado anakunjwa tu na makada wenzake wa ACT-Tanzania
     Alipotafutwa Mwigamba na Chanzo changu kimoja  huku akizungumza kwa uchaungu alidai vijana haowamekodiwa na Limbu kwa lengo la kumfanyia vurugu baada ya kuona mikakati yake imekwama ndani ya chama.

“Limbu alikuja na kundi la vijana kama 12, kati yao wawili aliwasafirisha kwa ndege kutoka Arusha na mmoja anaitwa Gerald Emmanuel, pia alikuwamo Mwenyekiti wa Geita, Katibu Uenezi Ukonga, Katibu Uenezi Jimbo la Kinondoni pamoja na kina Mahona.
Gafla akatokea  kiongozi mwengine wa ACT-Tanzania kuja kumgombelezea

          “Sasa wakati bado hatujaingia ofisini kwa msajili tukaambiwa tunatakiwa mimi na Limbu tu ndio tuingie na wengine waondoke, lakini kikundi cha Limbu hakikuondoka wakabaki pale nje wanajadiliana,” alisema Mwigamba.
Alisema wakati wamemaliza kikao na msajili, alifuatwa na Gerald huku akimshika shati lake na kumwambia anamdai fedha zake Sh milioni moja, hivyo lazima amlipe.

Wakatokea Viongozi wengine wa ACT-Tanzania ambao wanamdai wakaanza kumshushia kichapo

          “Wakati tunatoka kikaoni nikawa pale nje nasubiri gari linichukue, akaja Gerald huku akishika shati langu akidai ananidai shilingi milioni moja na lazima nimlipe pale pale, nilishangaa sana na hapo ndiyo nikajua kuna kitu Limbu amefanya ili wale vijana wanivuruge na baadaye nikasirike na kuonekana nimepigana,” alisema Mwigamba
    
  Baada ya Tambwe hizo za mwigamba zisizokuwa na ushahidi wa moja kwa moja,chanzo changu kilimtafuta na Mwenyekiti wa chama hicho cha ACT-Tanzania Kadawi limbu  aliyefukuzwa na Ghiriba za Mwigamba na wezake alisema-
       hakuona vurugu hizo kwani wakati huo alikuwa anazungumza na simu pembeni, na kwamba Gerald na Mwigamba wanajuana kwa kuwa wote wanatoka Arusha.
       
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, alisema hakushuhudia fujo hizo na kusema kwamba kuna watu wanataka kuvuruga mazungumzo yake na ACT.
“Kuna watu wanataka kuyavuruga haya mazungumzo, ndio haohao ambao wanasambaza hata picha huko kwenye mitandao ya kijamii na kukuza mambo,” alisema Jaji Mutungi.
          Kuibuka kwa Mgogoro katika chama hicho inadaiwa kuwepo viongozi wawili wa chama hicho wakiongozwa na Profesa Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba wote kwa pamoja walifukuzwa chadema kutokana na Usaliti na kukimbilia katika chama cha ACT-Tanzania ambapo sasa wameupindua uongozi uliopo sasa.
      Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali zinasema lengo la wawili hao ni kumpindua mwenyekiti  wa Chama hicho Bwana Limbu katika nafasi hiyo ili-
       
Mwanachama mwenzao aliyefukuzwa na Chadema Zitto Kabwe ashike nafasi ya Limbu.
          Zitto,ambaye ni mbunge wa Kigoma kaskazini,alifukuzwa Chadema yapata mwaka Mmoja sasa,na tangu hapo amekuwa akifahamika kuwa mwanzilishi au “mwanachama wa kimyakimya” wa ACT
           “Umoja huu kati ya Profesa Kitila na Mwigamba umelenga kukiua chama chetu na sisi hatutokubali lazima tuwafukuze,maana tunajua viongozi hawa wameunda umoja eti kupambana Limbua aondoke ili wamelete huyo Zitto na sisi hatubali”alisema Kiongozi Mwanzilishi wa chama hicho ambae akutaka jina lake litajwe

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.