TIZAMA UKAWA KIGOMA WANAVYOFURAHIA MGOGORO WA ACT TANZANIA

Ni wazi inaaminika kuwa ngome kuu ya ACT Tanzania ipo Kigoma ambapo ndipo inasadikika kuwa mizizi ya ACT Tanzania imewekwa hapa,leo mwandishi wetu alitembelea kijiwe cha wakereketwa wa UKAWA kinachofahamika kwa jina maarufu kama ''Urusi Asili'' na kukuta ujumbe mzito uliosomeka hivi:-

ACT wazichapa kavukavu!!! mbele ya msajili wa vyama wakionyeshana umwamba wao.ataeshinda ndie atakuwa mwenyekiti wa chama.au hiyo ndio Demokrasia ya kweli? watu wazima kuzichapa hadharani? amaakweli siku zote wasaliti hawana mafanikio.Vipi tena sio Taifa kwanza? leo hii imekuwa chama kwanza??...Sawfa Taalamuuna Chadema ..

Huku katika kijiwe halisi cha ACT kukiwa hakuna ujumbe wowote kama ilivyozoeleka,pia katika maandishi hayo waliambatanisha picha iliyozagaa kwa kasi jana mitandaoni kama inavyoonekana hapo kwenye ujumbe waliouandika ikimuonyesha katibu wa chama cha ACT Tanzania Samson Mwigamba akishikwa shati na mtu ambae hakufahamika jina maramoja,ikumbukwe kuwa Kigoma ni moja ya mikoa michache Tanzania aliyobeba historia za kisiasa nchini Tanzania toka mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa,kwani umekuwa mkoa ambao ukitoa watu na wanasiasa ambao wamekuwa wakiitikisa Tanzania.
Tawi hili la UKAWA ambalo linafahamika kama ''Urusi Asili'' lilitokana na mpasuko pale alipovuliwa nyadhifa katika chama cha Chadema mh.Zitto Zuberi Kabwe,ndipo jina ''Urusi Asili'' likapatikana kwani awali kabla ya mpasuko ilikuwa ikifahamika kama ''Urusi Yenye Nguvu'' ,pia matawi yote haya mawili yapojirani kabisa na pembezoni mwa barabara ya Mwanga Kigoma mjini

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.