OMARY KATANGA WA E FM APATA SHAVU LINGINE

NA KAROLI VINSENT


      ALIYEKUWA Mtangazaji wa kipindi cha Michezo ndani ya Redio one ambaye sasa ni Mtangazaji wa Redio mpya ya E.FM Omary Katanga amepata shavu jingine,baada ya kuteuliwa kuwa Afisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dar es Salam (DRFA).
     
    Awali nafasi hiyo ya Afisa Habari kwenye chama hicho alikuwa inashikiliwa  na Mohamedi Mwalizo ambaye mkataba wake imekwesha.
     
Akitambulishwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari na katibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam Msanifu Kondo alisema kuchaguliwa kwa Katanga katika nafisi hiyo kumetokana na kutambua mchango wake katika kutoa taarifa kwa umma ikiwemo na umakini aliokuwa nao.
     
        “Katika kikao cha kamati kilichokaa tumefikia hatua ya kumchagua Omary Katanga kuwa Afisa Habari katika chama hichi ili aweze kutupa urahisi wakuwapa taarifa wanamichezo pamoja wapenzi wa mkoa wa Dar es Salaam”alisema Kondo.
        

         Kondo aliongeza Chama hicho kinampongeza aliyekuwa Afisa Habari wa chama hicho Mohamedi mwalizo kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili na akawataka wanahabari kumpa ushirikiano Katanga katika kazi
      
     Kwa upande wake Afisa huyo habari mpya Omary Katanga alishukuru kwa kuchaguliwa katika nafasi na kusema ataitumikia kwa moyo wote na kuwataka wanahabari wenzake wampe ushirikiano kuboresha mpira,
     
          Kuhusu Mkataba wake na Redio E.Fm ambayo sasa anaitumikia alisema ataendelea kufanya kazi Redio hiyo kwani aimzuii kufanya kazi na DRFA.
        
        Kwa upande Mwengine DRFA wamesema kwa sasa wako katika kozi ya Madaktari wa michezo inayotarajiwa kuanza kuanzia 23 mwezi huu hadi tarehe 27 pia mwezi huu,huku pia kukiwa na kozi nyingine ya masuala ya utawala na washiriki wa kozi hiyo watakuwa wajumbe wa kamati ya utendaji wa DRFA na Maafisa  wa michezo wa  manispaa watendaji

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.