Saturday, January 3, 2015

ZIARA YA RIDHWANI ILIYOACHA GUMZO HUKO CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.

Watioto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea mnara
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi  kuboresha barabara na mawasiliano ya simu
Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Kwa Mduma wakati wa ziara yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata ya Kibindu

No comments: