Sunday, February 1, 2015

HABARI MPYA--LIPUMBA AJITOKEZA MBELE YA WANAHABARI LEO,SOMA ALICHOKIZUNGUMZA

Mwenyekiti wa profesa  CUF IBRAHIM LIPUMBA akiwasili katika mkutano huo na wanahabari muda mfupi uliopita
Kwa mara ya Kwanza tangu kutokea kwa vurugu za kisiasa ambazo zilisababisha mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIM LIPUMBA kupigwa na kukamatwa na jeshi la polisi na hatimaye kupelekwa mahakamani mwenyekiti huyo amejitokeza leo jumapili mbele ya wanahabari na kueleza hali halisi ya tukio hilo huku akieleza adhma yake ya kutaka kumuona rais kikwete kumueleza matatizo ambayo polisi wa Tanzania wanayo ambayo yanapaswa kuzibitiwa mara moja.

Akizungumza kwa uchungu mkubwa LIPUMBA amesema kuwa kilichotokea juzi huko mbagala ni ishara tosha kuwa Tanzania hakuna amani na democrasia ya kweli kwani kuzuia maandamanao ambayo kila mwaka huwa yanafanyika kwa amani na utulivu ni kuwanyima haki watanzania ya kuwakumbuka ndugu zao waliofariki katika vurugu za Zanzibar.
Amesema kuwa kitendo walichokifanya polisi kimewasikitisha sana wao kama wapenda amani na haki kwani polisi hao walikuwa na taarifa tangu tarehe 22 mwezi wa kwanza ila wao wakaja kupiga marufuku maandamano hayo terehe 26 jioni jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani hawakuwa na muda wa kuwaambia wanachama wao kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku.

“sasa nafanya utaratibu wa kistaarabu kabisa wa kwenda kuonana na rais kikwete na lengo langu ni moja tu la kutaka kumueleza uhalisia wa jeshi la polisi na vitendo vibaya wanavyovifanya kwani tukiendelea kufumbia macho matukio kama haya mwisho wa siku tutajikuta mahali pabaya sana sisi kama nchi hivyo nataka kumueleza kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee.”amesema lipumba.

Aidha akizungumzia kauli ya serikali iliyotolewa bungeni na waziri wa mambo ya ndani mh MATHIAS CHIKAWE kuwa CUF walikaidi maagizo ya polisi ya kusitisha maandamano na ilikuwa ni njia ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa amesema kuwa ni kauli za kutunga na uzushi mkubwa na kauli hizo zimeonyesha ni jinsi gani serikali imedhamiria kuwapiga wananchi kisawa sawa katika matukio kama hayo.

Mnamo tarehe 27 mwezi wa kwanza CUF walikuwa wafanye maandanano ya amani kuwakumbuka wanachama wenzao waliouawa huko zanzibari lakini maandamano hayo yaliishia mikononi mwa jeshi la polisi huko mbagala.

Aidha amewashukuru sana watanzania hususani vyombo vya habari kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika sakata hilo na kuuweka ukweli wa jambo hilo wazi ambapo kila mtanzania ameweza kufahamu ni nini kimetokea.



No comments: