Sunday, February 1, 2015

WIKI YA SHERIA NCHINI YAZINDULIWA,LHRC WASHIRIKI KIKAMILIFU,RAIS MWINYI AZINDUA REPORT MBILI ZA KITUO HICHO,TUKIO NZIMA LIKO HAPA

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akizindua ripoti ya utafiti wa utendaji kazi wa mabaraza ya Kata ya Ardhi kwenye banda la Kituo cha Sheria na haki za Binadamu wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kinashiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambayo yanafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dare s salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa utoaji haki nchini ambapo LHRC ni moja kati ya wadau hao.

Katika maadhimisho hayo ambayo yamezindiliwa leo na rais mstaafu wa awamu ya pili mzee ALLY HASSAN MWINYI yemeenda sambamba na uzinduzi wa report mbili za LHRC zinazoonyesha mwenendo wa kesi ambazo kituo hicho kinapokea na kesi za ardhi ambazo zinarepotiwa katika kituo hicho.
Akizungmza na mtandao huu katika banda la kituo hicho ndani ya viwanja vya mnazi mmoja afisa program dawati la ufwatiliaji na utendaji wa mahakama Bi ROSEMARY MANASE amesema kuwa kituo hicho kimezindua report mbili ambayo moja inaonyesha aina ya kesi ambazo zimeripotiwa kwao  na ambazo wameshughulika nazo report ambayo amesema kuwa wataisambaza kwa wadau wote kwa lengo la kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi pamoja na kutoa elimu kwa watanzania.
Watoa huduma wakiwa tayari kutoa maelekezo kwa wananchi watakaotembelea banda lao kayika maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam
Afisa huyo amesema kuwa katika kazi zao za kushughulika na kesi mbalimbali mkusanyiko mkubwa kesi umekuwa katika kesi za ardhi na kesi za madai ambapo amesema kuwa kunahitajika nguvu ya ziada katika kushughulika na kesi kama hizo kwani zimekuwa ndio nyingi kwa watanzania.
Mwanasheria kutoka LHRC ndugu HAROLD SUNGUSIA akitoa maelezo kwa wanahabari waliotembelea banda lao juu ya report hizo mbili zilizozinduliwa katika maonyesho hayo
Akizitaja changamoto ambazo wanakumbana nazo katika kutoa msaada wa kisheria ameseama kuwa elimu ndogo ya kisheria kwa wanachi,watu kuwa na hofu na mahakama zetu,mahakama chache pamoja na kucheleweshwa kwa kesi nyingi imekuwa ni kikwazo kikubwa katika secta hiyo ya sheria hapa nchini.

Maadhimisho yato yanafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo wadau mbalimbali wa maswala ya kisheria wanakutana katika maonyesho hayo.
Wananchi wanaojitokeza katika banda hilo


No comments: