Wednesday, February 25, 2015

HII NI KALI LEO KUTOKA KWA CHENGE NA ESCROW LEO

Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi ,
Andrew Chenge akitoka kwenye Kamati ya Maadili leo Jiji Dar Es Salaa

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Magharibi,Andrew Chenge amesema anataka muongozo wa kujadiliwa yeye katika Tume ya Maadili kutokana na suala la Akaunti ya Tegeta Escrow liko Mahakamani hivyo shitaka lake haliko msingi wa kisheria ,Anaripoti KAROLI VINSENT ,Endelea nayo ..

Kugoma kwa chenge kwa shitaka lake kutosikilizwa na  kutaka Tume ya Maadili itolee ufafanuzi juu ya kuwepo kwa Shauri kwenye Makama kuu ya Tanzania linalozuia kujadiliwa kesi nje ya Mahakama hivyo kuhusu sakata la Akaunt ya Tegeta Escrow kumetokea mda huu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anasomewa mashtaka yake kwenye tume hiyo ambapo---..
                
Chenge ambaye ni Mwanasheria Mkuu  wa zamani wa Serikali anashatakiwa na tume ya maadili kutokana na kitendo chake che kupokea pesa ya zaidi Bilioni 1.6.8 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering bwana James Rugimalira wakati akiwa mtumisha wa umma na bila kuitangaza kama zinavyodai sheria za tume hiyo.
             
  Mbunge huyo alipandishwa Mahakama ya Baraza la maadili mda huu Jijini Dar es Salaam mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo maadili Jaji Mstaafu Hamis Msumi -
           
 Ambapo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Baraza Maadili Hassan Mayunga  alidaiwa Mbunge huyo wakati akiwa mwanasheria mkuu wa serikali mwaka 2006  alivunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuipa mkataba wa Miaka 20 kampuni ya kufua Umeme ya IPTL.
           
Wakili huyo amesema kitendo iko cha Chenge kuipa mkataba kampuni hiyo kinaonekana wazi alikuwa anamaslahi yake binafsi kwenye kampuni hiyo  na kupelekea kuingiziwa pesa na Mbia wa Kampuni ya IPTL ambayo ni VIP Engineering na kupata mgao wa bilioni 1.6.8 kama zawadi ya kuingizia hasara serikali kwenye mataba hao.
Mbunge Chenge akimgomea mwandishi wa habari wa
 Itv na Radio One Ufoo  asimuulize swali lolote
    Mabishano ya Sheria yatokea
Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo na Wakili huyo wa Baraza hilo ndipo Chenge akaliomba Baraza hilo lisijadili kesi hiyo kutokana na kuwepo kwa kesi mahakama kuu linalokataza Vyombo vyovyote vya Serikali visijadili suala linalohusu Mihamala ya Akaunt ya Tegeta Escrow mpaka pale hukumu itakapotolewa.
Baada ya kusema hivyo Mwenyekiti wa Baraza hilo JajiHamis Msumi

Alimtaka Wakili wa Baraza hilo kuhakiki hati ya Staka ya mahakama kuu na Wakili huyo akajitetea na kusema hakuna kipengere kwenye kesi hiyo iliyoko mahakama kuu kinachozuia vyombo vingine kuzungumzia.
Baada ya kusema hivyo Jaji Hamis Msumi h akahahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili apate mda wa kusoma hati hiyo ya mahakama kuu kama kutakuwa na kipengele hicho kwenye kesi na endapo kitakuwepo basi Tume hiyo haiwezi kulizungumzia suala hilo

No comments: