Wednesday, February 18, 2015

KUHUSU KUKATWA KWA MAJI DAR ES SALAAM

DAWASCO YATOA TAARIFA YA KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU

SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM (DAWASCO) INAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA KIBAHA MKOANI PWANI KUWA MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU JUU UTAZIMWA KWA WASTANI WA SAA 12 KUANZIA SAA 12:00 ASUBUHI HADI SAA 12:00 JIONI KWA SIKU YA IJUMAA 20/02/2015.

MTAMBO YA RUVU JUU UTAZIMWA ILI KUMRUHUSU MKANDARASI KUFANYA SHUGHULI ZA UPANUZI WA MTAMBO.

KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU KUTASABABISHA MAENEO YAFUATAYO KUKOSA MAJI;

MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, KILUVYA, KONGOWE, MISUGUSUGU, VISIGA, TONDORONI,KIMARA BARUTI, BAHAMA MAMA, UBUNGO, MSEWE, CHUO KIKUU, KOROGWE, GOLANI, KIBO, MAVURUNZA, UBUNGO MAJI, TANESCO, KIBANGU JUU, TABATA (MAWENZI, KISUKURU, CHANG’OMBE, KIMANGA, SEGEREA.

MAENEO MENGINE NI BONYOKWA, MAKOKA, KILUNGULE, 770, MANDELA ROAD, MABIBO HOSTEL, KIBANGU CHINI, MAKUBURI, TABATA (KISIWANI, MATUMBI, BIMA NA DARAJANI).

DAWASCO INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA


KWA TAARIFA ZAIDI PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022-2194800 /

 0658-198889

.IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO- MAKAO MAKUU

No comments: