Thursday, February 19, 2015

KUTOKA TIGO LEO,NAO PIA WAZUNGUMZIA KUPUNGUZWA KWA VIFURUSHI,WAJIPANGA PIA KUJITANUA ZAIDI MWAKA HUU

 Meneja mkuu wa tigo Tanzania CECILE TIANO akizngumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam
Kampuni ya mawasiliano ya tigo nchini Tanzania imepanga kutumia million 120 za kimarekani sawa na 221bn mwaka huu katika kupanua mtandao wake na kuimarisha kiwango cha ubora wa huduma zake.

Akieleza mipango ya kampuni hiyo kwa mwaka 2015 kaimu meneja mkuu wa tigo Tanzania CECILE TIANO amesema kuwa kiasi hiki cha uwekezaji ni ongezeko la asilimia 20 kutoka dola za kimarekani 100 sawa na 184bn ambazo kampuni hiyo iliwekeza mwaka jana katika upanuzi na uimarishaji wa mtandao wake wa mawasiliano.

Amesema kuwa ongezeko la uwekezaji linaonyesha juhudi za kampuni hiyo kwa wateja wake na kiwango cha huduma zao ambacho ni zaidi ya matarajio yao na pia inawapa watanzania fursa ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu ndani ya nchi.

Kulingana na maelezo yake anasema kuwa mwaka 2014 ni msimu uliokuwa wa mafanikio ambapo tigo ilijivunia record ya asilimia 30 kwa ongezeko kwa wateja wake waliojiunga mwaka jana ilipelekea idadi ya wateja kuongezeka kutoka million saba hadi million tisa.

Aidha amesema kuwa kampuni ya tigo Tanzania inataka iendelee kutanua wigo wa mtandao huo kwa kuweka minara 787 mipya nchini nzima na baadhi ya minara hiyo itakuwa na 3g na 4g . ambapo amesema kuwa minara hiyo itapelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa uduma za tigo vijijini na pia itaongeza upatikanaji internent wa wateja wa mtamndao huo.ambapo amesema kuwa tigo kwa sasa ina minara 2,000 nchi nzima
Bi TIANO amesema kuwa mipango mingine ya kampuni hiyo kwa mwaka huu ni kuhusu kuongeza mara mbili idaadi ya maduka ya huduma kwa wateja kutoka maduka 42 mpaka maduka 100 katika kuhakikisha kuwa huduma hizo zinawafikia wateja wengi nchini.

Aidha akijibu swali la mwandishi wa mtandao huu kuhusu kupungua ghafla kwa vifurushi vya mtandao wa internent bila taarifa mkurugenzi huyo ameesema kuwa Tanzania bado ni nchi ambayo ina gharama za chini sana katika matumizi ya internent ukilinganisha na nchi nyingine za Africa ambapo amesema pia chanzo kingine cha kupunguza huduma hiyo ni kutokana na tozo kubwa ya kodi wanatotozwa na serikali kwa sasa ambapo amesema hata hivyo sio muda muafaka wa kulizungumzia swala hilo kwani tayari wamepata malalamiko kutoka TCRA kuhusu kukatisha huduma hizo bila taarifa na wapo katika mazungumzo na waatanzania watajuzwa kinachoekndelea
                                          

No comments: