Wednesday, February 4, 2015

MAANDAMANO YA CCM YAPIGWA STOP


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam leo limesitisha maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es salaam na umoja wa vijana wa chama cha mapindiuzi CCM  hapo kesho.


Akizungumza na wanahabari mapema leo kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam SELEMAN KOVA amesema kuwa uamuzi wa jeshi hilo kusitisha maandamano hayo inatokana na taarifa za kiinteligensia ambazo wamezipata zikieleza kuwa maandamano hayo yatahusisha makundi mbalimbali kama bodaboda,mama ntilie,jambo ambalo amekiri kuwa halikuwepo kwenye maafikiano yao.

Kamishna kova ameeleza kuwa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ilala uliliandikia jeshi hilo barua kuwa mnamo tarehe tano mwezi huu watakuwa na maandamano ya amani yatakayoanzia katika ofisi za chama hicho zilizopo lumumba hadi viwanja vya jangwani Jijini Dar es salaam ikiwa ni kuazimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo jeshi limebaini kuwa kuna uwezekano wa vitendo vya uvunjifu wa amani na kuamua kuyasitisha.

Aidha kamishna kova ameeleza kuwa jeshi hilo limebaini ushiriki wa makundi mbalimbali katika mkutano huo na kuangalia ujumbe ulioandikwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwaita viongozi wa chama cha boda boda na kuonyesha nia ya kushiriki kwenye maandano hayo kama yangekuwepo.


Amesema kuwa shughuli nyingine za maadhmisho hayo zinaruhusiwa kuendelea lakini sio maandamano hayo kwa kuwa yanekiuka baadhi ya makubaliano.

No comments: