Friday, February 13, 2015

MAANDAMANO YA CUF KIMYAA--KOVA AIBUKA KIDEDEA

Pichani ni Kamishna wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman kova picha na maktaba

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuthibiti maandamo ya Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha wananchi (JUVICUF) yaliyopangwa kufanyika leo Jijini Dar es Salaam, baada ya mwenyekiti wa Chama hicho profesa Ibrahimu Lipumba kukubali yaishe.Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
       
Kufanikiwa huko kwa Jeshi la Polisi kuthibiti maandamano hayo kunamaliza Vita iliyotangazwa jana na mwenyekiti wa JUVICUF ambaye alitangaza maandamano kuanza makao makuu ya chama hicho zilizopo Buguruni Jijini hapa hadi  ofisi za wizara ya mambo ya Ndani zilizopo Posta , huku wakijanadi hawatamuogopa Polisi yeyote.

        
 Akithibitisha kuthibiti maandamano Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova  leo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,ambapo Kamishna Kova huku akiongea kwa madaha amesema  Jitahada za jeshi la hilo la polisi wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuthibiti maandamano hayo kutokana Jitahadi kati yake Kamishana Kova na Mwenyekiti wa CUF profesa lipumba baada ya kuona maandamano hayo yataharibu amani ya nchi.
     
   Kanishna Kova ameongeza kuwa baada ya kufanya mawasiliano na Profesa Lipumba na kuongea nae kwa mda mrefu huku wote kwa pamoja wakizungumzia madhara ambayo yatatokea baada ya maandamano hayo kufanyika,ndipo Profesa Lipumba akabaini maandamano hayo yatakuwa na madhara makubwa ikiwemo kuleta machafuko pamoja na vurugu .
      
 Aidha,Kamishna Kova amesema kuwa hali ya  Amani katika Jiji la Dar es Salaam sio nzuri kufanya maandamano na  pindi jeshi la polisi linapozuia maandamano hayo hawafanyi kwa ajiri ya kuzorotesha siasa nchini bali wanafanya hivyo ili kurinda amani ya nchi ambayo inaweza kuharibika  kwenye maandamano hayo.
     
 Alibainisha, kuwa kwa sasa maandamano na mikutano yenye lengo la kuvuruga amani hayatakubalika na hivyo jeshi la polisi litalazimika kutumia uwezo wake wote wa kisheria kuyadhibiti kwa mbinu mbalimbali.
           Vilevile Kamishna Kova aliwashukuru Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Lipumba kuonyesha Busara ya hali ya juu baada ya kubaini kwamba kufanyika maandamano hayo yangesababisha madhara makubwa ikiwemo umwagikaji wa damu na wakati mwengine kwa watu ambao hawahusiki na usumbufu huo.

   PROFESA LIPUMBA ANENA.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu lipumba akiyahahirisha maandamano hayo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni leo Jijini Dar es Salaam aliwataka  wanachama wa chama hicho popote walipo kuacha kufanya maandamano hayo kutokana na kubaini kuwa kutakuwa na uvunjifu wa Amani.

No comments: