Friday, February 27, 2015

MAPYAA---DC MAKONDA KUPANDISHWA KIZIMBANI RASMI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa dare s salaam bwana JOHN GUNINITA leo ametangaza kumpandisha mahakamani mkuu wa wilaya ya kinondoni  DC PAUL MAKONDA kwa kila elichokiita kuwa ni kudhalilishshwa na kutupiwa maneno ya kashfa.VIDEO IKIONYESHA SIKU MAKONDA ALIPOTOA MANENO HAYO
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dare s salaam mh GUNINITA amesema kuwa kitendo alichokifanya DC MAKONDA cha kuitisha mkutano wa wanahabari na kuwatukana viongozi wastaafu wa chama cha mapinduizi ni kitendo ambacho hakivumiliki na mtu yoyote na kwa kuwa chama kimeshindwa kumshughulikia sasa njia pekee anayoiona inafa kumwadhibu ni kwenda mahakani ili haki ipatikane.


Amesema kuwa sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa kiongozi wa umoja wa vijana CCM kulalamikiwa kwa kitendo chake cha utomvu wa nidhamu mbele ya viongozi wenzake wa ndani ya chama hivyo sasa ni wakati muafaka wa kuhakikisha kuwa wanamfundisha adabu kwa kutumia sheria za Tanzania.

Ameongeza kuwa chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kuwaonya wanachama wake pale wanapokwenda kinyume na utaratibu wa chama hicho lakini kitendo cha kijana huyo kutoka nje mbele ya wanahabari kuwatukana viongozi wa chama hicho ambao mbali na uongozi ni baba zake ni kitendo ambacho sio utaratibu wa chama na hakina wa kuvumilia kitendo hicho

“sisi sio wa kwanza kutukanwa na MAKONDA,alianza kututukana sisi na viongozi wengine,juzi amemtukana waziri mkuu mstaafu na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba tanzania jaji JOSEPH WARIOBA na akaona haitoshi tumeshughudia akimpiga katika mkutano ambao yeye alienda kama mwalikwa tu ni utomvu wa nidhamu wa hali ya juu na siamini kama chama kjimemwacha kama alivyo”amesema GUNINITA.
Amesema kuwa MAKONDA ni kiongozi mdogo sana kwani nafasi aliyokuwa nayo umoja wa vijana UVCCM yeye amekaa hapo kwa miaka kumi na nafasi yake mpya ya ukuu wa wilaya yeye amekaa miaka 25 hivyo asitumie vyeo vyake vya kuoteshwa kama uyoga kuwatukana wakubwa ndani ya chama hicho.
Paul makonda aliitsha mkutano wa wanahabari ambapo aliwatuhumu mwenyekiti huyo mstaafu pamoja na viongozi wengine wastaafu wa chama hicho akiwemo mzee msindai kuwa ni vibaraka wanaotumwa na baadhi ya wasaka uraisi kukivuruguga chama cha mapinduzi.

KUHUSU CHAMA CHA MAPINDUZI
GUNINITA amesema kuwa chama cha mapinduzi kwa sasa kimekuwa ni chama cha wakubwa na kupeana vyeo hivyo watu kama yeye hata walalamike hadi mwisho hakuna wa kuwasikiliza tena na amejaribu kulalamika kwa viongozi wa juu wa chama kuhusu MAKONDA lakini hakuna aliyemsikiliza na ndio nmaana ameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake.

MWANASHERIA ALONGA
Naye mwanasheria ambaye anashgulika na kesi hiyo BENJAMEN MWAKAGAMBA amesema kuwa mteja wao ameleta malalamiko ya kulalamika kuwa amedhalilishwa kwa maneno hivyo wao kama wanasheria wameona kuwa ni kweli kuwa mteja wao amedhalilishwa sana hivyo wameamua kwenda mahakamani kumshaki MAKONDA.

Amesema kuwa baada ya kauli hizo za kongozi huyo wao kama wanasheria walimwandikia bariua ya kumtaka aombe radhi mbele ya vyombo vya habari pamoja na kulipa faini ya million mia moja lakini aliwajibu kuwa kauli hizo hakuzitoa yeye bali ni maagizo kutokia kwa viongozi wa juu wa chama hicho hivyo hawezi kuomba radhi kwa kauli hizo.

No comments: