Friday, February 27, 2015

WATU 14 MBARONI KWA UTEKAJI WA ALBINO TANZANIA

Watu wenye ulemavu wa ngozi waendelea kuishi kwa hofu nchini Tanzania.
Watu wenye ulemavu wa ngozi waendelea kuishi kwa hofu nchini Tanzania.

Mwanza, Jeshi la polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji nyara wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Pendo Emanuel wa kijiji cha ndami wilayani kwimba tukio  lililotokea Desemba 27 mwaka jana.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za Misungwi, Kwimba na Sengerema Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa mulongo  amesema kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao wamo waliohusika kwenye utekaji wa mtoto huyo pamoja na wale waliomuhifadhi kwenye hoteli moja jijini Mwanza kabla ya kumsafirisha kwenda kusikojulikana.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza Alfred Kapole pamoja na katibu wa chama hicho mkoani humo Enos Tuju wameendelea kukemea  ukatili dhidi watu wenye ulemavu wa ngozi Albino  pamoja na  kuiomba serikali kudhibiti vitendo vya mauaji  ya albino yanayo  endelea kutokea mkoani Mwanza.

No comments: