Sunday, February 1, 2015

TIGO KUWEKEZA DOLA MILLION 30 KANDA YA KASKAZINI MWAKA 2015

Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania Cecile Tiano(kulia) akiongea na waandishi wa habari Mkoani Arusha(hawapo pichani), wakati wa kutangaza kuongeza kwa uwekezaji wa dola za kimarekani milioni 30 kwa mikoa ya kanda ya Kaskazini mwishoni mwa wiki, kulia kwake ni Meneja Mkuu wa kanda hiyoDavid Charles.
Kaimu Meneja mkuu wa Tigo Tanzania, Cecile Tiano,ameelezea nia ya kampuni yake kuongeza uwekezaji katika mikoa ya kanda ya kaskazini kwa kiasi  cha dola za kimarekani milioni 30 alipokuwa akiongea nawaandishi wahabari mjini Arusha.
Tiano, aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi huu, ameisifu kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Singida, Dodoma na  Kilimanjaro kuwani eneo la kibiashara na utalii bila kusahau kuwa ni njia kuu ya kuelekea mataifa jirani. 
Alifafanua kwambaTigo inajumala ya minara 334 katika ukanda wa kaskazini ikiwemo 71 iliyojengwa mwaka 2014.Mwaka jana Tigoi lijenga jumla ya minara 312 nchi nzima.

 “Mwaka huu tumepanga kujenga minara mingine 748 nchima nzima ambayo 300 itakuwa katika kanda ya kaskazini ilikuhakikisha wakazi wa vijiji vya mikoa yote mitano wanaunganishwa na huduma zetu. Kwa wastani wadola 100,000 kila mnara, hii inamaanisha uwekezaji wazaidi ya dola milioni 75 nchi nzima ikiwemo dola milioni 30 katika mikoa hii mitano.," Alisema.

“Hii inamaanisha watu wengi zaidi watapata fursa mpya za kijamii na kiuchumi, wakiunganishwa katika uchumi wakidunia kupitia mtandao waintaneti – na kwa kufanya hivyo tunawawezesha kujiunga na mfumo mpya wa digital,” alisisitiza Tiano.

Kanda ya Kaskazini pia imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na mipango kadha ya udhamini na miradi ya kijami ikutoka Tigo, miradi ambayo Tiano alisema inalengo la kuleta mageuzi chanya katika Nyanja za elimu, afya, mazingira, ujasiriamali (ajira), sanaa na michezo.
“Kupitia juhudi zetu kama zile za mashindano ya Tigo Ngorongoro Run, mbio ambazo zimekuwa zikifanyika Karatu kila mwaka, kampuni yetu, pamoja na wadau wengine,tumeweza kukusanya fedha ambazo hutumika kununulia vyandarua shuleni, vifaa vya hopitali mbalimbali katika wilaya ya Karatu,”alisema.
Katika hatua nyingine Tiano ametangaza udhaminiwa Tigo kwambio za marathoni za Kilimnajaro mwaka huu kwa kiasi cha shilingi milioni 80. Mbio hizo zitafanyika tarehe 1 Machi 2015 ambapo Tigo inadhamini nusu marathoni ya kilomita 21, alisema
“Sababu ya Tigo kujiingiza katika mashindano haya ni kuonesha nia yake ya kuendeleza sekta ya michezo na Nyanja nyingine za kijamii na za kiuchumi katika nchi hii, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Tigo imekuwa ikiwekeza kwenye miundo mbinu yake kwa wastani wa dola milioni mbili kwa wiki nchi nzima. Uwekezaji huu, kwa mujibu wa Tiano, umesaidia kupanua mtandao  wake mpaka sehemu za vijijini; kuboresha mtandao wake hadi kufikia vipimo vya 3G hivyo kuwa wezesha wateja kupata huduma ya  Internet; kuelimisha wafanyakazi wake na kuleta manufaa kwa jamii kwa kuwekea katika miradi ya kijamii.

Tiano aliendelea kusema kuwa ndani ya miezi 12 iliyopita Tigo imekuwa kampuni ya kwanza kubni huduma mpya zikiwemo kutuma na kupokea pesa kutoka Rwanda kupitia TigoPesa; kuanzisha huduma ya bure ya Facebook kwa Kiswahili pamoja;na kuanzisha ushirikiano na kampuni nyingine za simu nchini kuwawezesha wateja kutumaau kupokea pesa kutoka mitandao hiyo. Mafanikio mengine ni kuwa wezesha wateja wake kuwekeana kutoa pesa kutoka akaunti zao za benki kupitia simu zao za mkononi; kwapa wateja gawio la faida itokanyo na utunzaji fedha zao katika akaunti zao za TigoPesa; na hivi karibuni uzinduzi wa huduma ya Tigo music inayowapa wateja wake fursa ya kufurahia muziki bila kikomo kupitia Deezer


No comments: