Sunday, February 8, 2015

WALE TUNAOPENDA SIMU ZA KISASA NA ZENYE UBORA,TIZAMA HII ILIYOZINDULIWA JANA DAR ES SALAAM

Watanzania mbalimbali waliojitokeza katika sherehe hizo ambazo zilifanyika usiku wa kuamkia jana jijini Dar es salaam
Kampuni ya kimataifa ya MICROSOFT MOBILE DIVICE jana imehitimisha kampeni yake kubwa aliyokuwa inaifanya katika nchi za afrika mashariki maarufu kama #MakeItHappen Campaign ambayo ilikuwa na lengo la kuwahamasisha wateja wa bidhaa zao kutumia kwa wingi simu zinazouzwa na kampuni hiyo kutokana na ubora wake.
 MICKA MAVOA ambaye ni country manager wa Microsoft mobile divice akizungumza na wanahabari baada ya shughuli hiyo 
Akizungumza na mtandao huu katika sherehe za kuhitimisha kampeni hiyo ambayo ilifanyika jijini Dare s salaam usiku wa kuamkia leo MICKA MAVOA ambaye ni country manager wa Microsoft mobile divice alisema kuwa kampuni yao kupitia LUMIA LIVING COMMUNICATION sasa wanalengo la kufanya ndoto za wateja wao kutimia na kuwa za kweli ambapo wameanzisha shindano ambalo mteja mwenye simu za LUMIA anaweza kutuma ujumbe mfupi akiielezea ndoto yake na kama ndoto hiyo itachaguliwa na kampuni hiyo basi wataifanya ndoto ya mteja wao huyo kuwa ya kweli.
Amesema kuwa cha kufanya ni kununua simu za LUMIA na kisha kutuma ujumbe mfupi wa maneno wa kuelezea ndoto zako na kuutuma kwenda 20096,ambapo unaweza kuchaguliwa katika wale ambao watatimiziwa ndoto zao kuwa za kweli.ambapo hii itawahusu wale ambao watanunua simu zao kuanzia 1st  Feb and 30th
March.

Wateja mbalimbali walipata nafasi ya kupata maelekezo kutoka kwa wauzaji wa LUMIA juu ya jinsi inavyofanya kazi na ubora wake kwa ujumla
Aidha katika sherehe hizo za aina yake zilishughudia uzinduzi wa simu mpya ya LUMIA 535 ambayo inauwezo mkubwa na wa kisasa na inakidhi mahitaji ya dunia ya leo.
Baadhi ya wateja na watanzania ambao walihudhuria katika hafla hiyo hawakusita kuzungumza na mtandao huu ambao wengi walionekana kufurahia simu ambazo zinatolewa na kampuni hiyo na kusema kuwa ni simu imara na bora ambazo zinamfaa kila mtanzania kwa kipindi hiki ambapo dunia imehamia kiganjani.
Mmoja wa wahudumu akiwa ameshika LIMIA 535 ambayo ndiyo ilizinduliwa jana ikiwa ni simu ya kisasa kuwahi kutokea Tanzania
Sherehe hizo ambazo zilifanyika jijini dare s salaam jana zilianza kufanyika katika nchi nyingine za Africa mashariki kama ugamda na hitimisho lake kuwa Tanzania jana. 
ENDELEA NA PICHA NYINGINE CHINI


Picha yatu zikionyesha jinsi sherehe hiyo ilivyofana ambapo wadau hapo wanaonekana wakiwa katika red carpet kupiga picha za kumbukumbu ya shughuli hiyo


No comments: