.

KUHUSU KAFULILA NA ACT LEO,SOMA HAPA


Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, amekanusha kuhamia chama cha kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).


Kafulula amesema kuwa hana sababu ya kuhama chama hicho na kukiri kuona katika mitandao ya kujamii habari kuwa anahama chama chake na kuhamia ACT jambo ambalo halina ukweli wowote.
Amesema kuwa huenda tetesi hizo zimekuja baada ya kuwa na marafiki wengi wa chama hicho na kusema kuwa urafiki na wanachama hao hauna maana kuwa anahamia chama hicho.
Hata hivyo Kafulila amehoji ana urafiki na wanachama wa Chadema, CCM, na vyama vingine mbona hawajavitaja, na kudai kuwa Zitto, amehama kutokana na kuwa na migogoro na chama chake lakini yeye hana sababu ya kuweza kukihama chama chake.
Ameongeza kuwa atabaki kuwa Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, na kuendelea na kampeni za kujenga chama hicho ikiwemo yeye kurudi bungeni pamoja na chama hicho kuongeza wabunge wengi zaidi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.