Thursday, March 5, 2015

PICHA--BARAZA LA MADIWANI TEMEKE WAKUTANA LEO KUJADILI MAENDELEO YAO




 STORY NA IZACK MAGESA
BALAZA la madiwani Halamshauri ya Temeke wamemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anatenga bajeti maalumu ili kunusuru jamii pindi ianapokumbwa na maafa mbali mbali.

Hayo yalisemwa Dar es salaam leo,wakati wa Balaza hilo lilikutana kujadili mambo mbali mbali yanayowahusu ikiwa ni moja ya mchakato wa kukuza maendeleo wilayani Temeke.

Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam leo.,Diwani wa kata ya Keko Francis Mtawa alisema lazima ifikie mahala Halmshauri iweze kutenga bajeti maalumu ya mahafa badala ya kutenga kitengo cha mahafa ambacho kipo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu Bw  Mizengo Pinda.

"lazima ifikie mahala na sisi kama Halmashauri iwe na bajeti ya mahafa badala ya kutegemea kitengo cha mahafa kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu,ambapo inakuchukua muda sana mpaka kuja kufikiwa 'alisema.
Madiwani mbalimbali kutoka manispaa ya temeke wakiwa wanaendelea na mkutano huo uliofanyika leo


 PICHA NYINGINE ZAIDI ZA MKUTANO HYUO ZIKO CHINI





No comments: