.

WATU WENYE UHITAJI MBALIMBALI WAPATIWA MISAADA JIJINI DAR ES SALAAMMwakilishi wa mkuu wa wilaya ya ilala bwana  JEREMIAH MAKORERE wa tatu kushoto akiwakabidhi watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama ALIBINO baadhi ya misaada ambayo imetolewa na taasisi hiyo kama njia moja wapo ya kusaidiana,hafla hiyo imefanyika jijini dar es salaamSTORY NA EXAUD MTEI

 Viongozi wa dini nchini Tanzania wameaswa kutumia muda mwingi katika kutoa elimu kwa waumini wao waachene na matendo mbalimbali yasiyo mpendeza mungu.

Kauli hiyo leo imetolewa na mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya ilala bwana JEREMIAH MAKORERE aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya ilala katika hafla fupi iliyoandaliwa na taasisi ya kiislam ya AL-MARID kwa ajili ya utoaji wa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji maalumu wakiwemo walemavu ambapo amesema kuwa kama maeneo ya ibada yatatumika ipasavyo yanaweza kuwabadilisha wananchi wakawa na roho ya kumuogopa mungu.
Baadhi ya waliopata misaada hiyo wakichambua kuona bidhaa walizopatiwa
Bwana MAKORERE amesema kuwa kumekuwa na matendo mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yanafanywa na watanzania wachache kutokana na kuwa mbali na mungu ambapo amezitaka taasisi mbalimbali za kidini kuwa katika mstari wa mbele katika kukemea hali hiyo.
Akitolea mfano wa mauaji yanayoendelea kushika kasi nchini tanzania ya watu wenye ulemavu wa ngozi amesema kuwa  pamoja na jitihadi kubwa zinazoonyeshwa na serikali ya tanzania katika kutoa elimu pamoja na kudhibiti bado  matendo hayo yanazidi kuongezeka kutokana na watu kutokuwa na hofu ya mungu hivyo akazitaka taasisi za kidini zote kwa umoja wao kuungana kuhakikisha kuwa hofu ya mungu inarejea mioyoni mwa watanzania ili kukemea matendo ambayo yanaonyesha kuvuruga amani ya Tanzania.
Mwakilishi wa mgeni rasmi bwana JEREMIAH MAKORERE akimkabidhi msaada kiongozi mmoja wapo wa kidini kutoka dhehebu la Budha, ambaye naye alifika katika hafla hiyo,hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi kutoka kila aina ya dhehebu nchini tanzania bila ubaguzi wa hali yoyote
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam taasisi ya kiislam ya AL-MARID imetoa msaada wenye thamani ya shilingi million 42 kwa makundi ya watu mbalimbali nchini yenye uhitaji maalumu wakiwemo walemavu wa ngozi,watoto yatima,wanafunzi na makundi mengine ambapo zaidi ya wahitaji 270 walikuwepo katika hafla hiyo kupokea zawadi hizo.
Baadhi ya misaada ikiwa tayari kutolewa kwa walengwa
Akizungumza na mtandao huu msemaji na muweka  hazina wa taasisi hiyo SHEKH RAJAB KATIMBA amesema kuwa  tasasisi yao imekuwa na utamaduni wa kutoa misaaada mara kwa mara katika makundi mbalimbali nchini ambapo kwa safari hii wamefanyia jijini dare s salaam na baadhi ya vitu waliivyotoa kama msaada ni pamoja na nguo,vyakula,vifaa vya wanafunzi vya shule,pamoja na misaada mingine ya kibinadamu.
About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.