Saturday, April 25, 2015

DIWANI WA CCM KIJICHI ATANGAZA NIA KWA STAILI YA AINA YAKE,TIZAMA ALICHOKIFANYA HAPA


Diwani wa kata ya kijiji Mh ANDERSON CHALLE akipiga mpira wa penalt kama ishara ya kuzindua rasmi mashindano hayo jana katika viwanja vya suhle ya msingi kijichi Jijini Dar es salaam
 Diwani wa kata ya Kiijichi kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mh ANDERSON CHALE amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu katika kata yake ambayo anayafadhili mashindani yatakayoshirikisha timu 60 kutoka katika kata hiyo mashindano ambayo yamepewa jina la UVCCM KIJICHI CUP
Alipata nafasi ya kukutana na timu mbalimbali ambazo zitashiriki katika mashindano hayo na kuzungumza na wachezaji hao ambao aliwataka kutumia mashindano hayo kama njia moja wapi ya kudumisha amani na mashikamano katika kata hiyo na njia moja wapo ya kujiletea maendeleo wenyewe
Akizindua mashindano hayo jana jijini Dar es salaam diwani huyo amesema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuwakusanya vijana na wananchi wa kata hiyo kwa pamoja ili kujenga umoja wa pamoja katika kuendesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika kata hiyo.
Mashindano hayo ambayo ni mara ya nne kufanyika na kudhaminiwa na Diwani huyo yanatarajiwa kugharimu zaidi ya Million 35 hadi kumalizika kwake ambapo diwani huyo amesema kuwa anafanya hivyo kutokana na nafasi yake aliyonayo kama Diwani ya kuwaleta wananchi pamoja na kujenga ushirikiano katika Kata hiyo.

Akizungumza na mtandao huu baada ya kufanya uzinduzi wa mashindano hayo ambao ulifanyika katika viwanja vya shule ya msingi kijichi Diwani CHALLE amesema kuwa lengo lake lingine ni kuona kuwa anakamilisha miradi mbalimbali ambayo amejiwekea katika kata hiyo ikiwemo ya maji,barabara na miradi mingine mingi ya kimaendeleo ambayo tayari ameianza ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza nia yake ya kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka huu ili kupata nafasi ya kuongoza kwa miaka mitano mingine aweze kumaliza kile ambacho alikianza.

Amewataka Wananchi kuendelea kumwamini na ikizingatia kuwa hii ni awamu yake ya kwanza kuiongoza kata hiyo ambapo amesisitiza kuwa anahitaji nafasi zaidi ya kuendelea kuongoza kata hiyo ili kuhakikisha kuwa anafikia malengo aliyojiwekea wakati anatafuta nafasi ya kuwatumikia wananchi hao.

Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi katika kata hiyo wakiongozwa na diwani wao Mh ANDERSON CHALLE wakishugudia moja kati ya michezo ya ufunguzi wa mashindano hayo






No comments: