Sunday, April 12, 2015

ILE TREN MPYA LEO INAENDA MWANZA,NI ILE ILIYOZINDULIWA WIKI ILIYOPITA


Uongozi wa kampuni ya reli nchini Tanzania TRL leo umetangaza kuanza kwa safari ya pili ya treni yake mpya  (DELUX) iliyozinduliwa mnamo wiki moja iliyopita ambapo safari hii ya pili itakuwa ni zamu ya kanda ya ziwa ambapo itaelekea mwanza leo tarehe 12,mwezi wa nne.

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam afisa uhusiano wa kampuni hiyo bwana MIDIADJY MAEZ amesema kuwa safari hii ni ya pili kwa vile uzinduzi ulishafanyika tarehe moja mwezi wa nne mwaka huu na kuelekea kigoma ziwa Tanganganyika ambapo treni hiyo ilipokelewa kwa furaha mjini kigoma na sasa ni zamu ya mkoa wa mwanza ambapo treni hiyo inafanya safari zake kwa wiki mara moja.
Afisa uhusiano wa kampuni hiyo bwana MIDIADJY MAEZ akizngumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam 
Amesema kuwa Treni hiyo mpya ya kisasa itakuwa ikifanya safari zake kwa wiki mara moja ambapo itakuwa ikiondoka Dar es salaam siku za jumapili kanzia saa mbili usiku ambapo itakuwa ikipokezana kati ya miji ya kigoma na mwanza.


Aidha akizungumzia habari ambazo zilisambazwa kuwa baada ya safari ya kwanza ya tren hiyo kulishughudiwa uharibifu mkubwa ndani ya mabehewa hayo ya kisasa amesema kuwa hakuna uharibifu mkubwa kama ilivyoripotiwa ila kilichotokea ni watu kutookuwa na elimu ya kutosha ya kutumia baadhi ya vifa vilivyo ndani ya treni hiyo ambapo amesema kwa sasa wamejipanga kwa kuwa na wahudumu wa kutosha ili kuhakikisha kuwa usumbufu kama huo hautokei tena.

No comments: