
Akitolea ufafanuzi wa
ugawanaji wa majimbo hayo alipokuwa anazugunmza na mtandao huu katibu mkuu wa
chama cha wananchi CUF MAALIM SHEIF SHARIF HAMAD amesema kuwa chama cha wananchi
CUF ni ukweli kuwa ndio chama chenye nguvu kwa upande wa Zanzibar ambapo kwa
pamoja walikubaliana kuwaachia CUF majimbo yote Zanzibar na ndipo chadema
wakaomba waachiwe jimbo la kikwajuni na ndipo wakawapa jimbo moja.
Amesema kuwa tayari
harakati za kuwapata wagombea wa ubunge katika kila jimbo visiwani zanzibari
kupitia chama hichi zimeanza ambapo hadi sasa kila jimbo limepata watu kama
saba ambao wanawania nafasi hizo na kinachofanyika sasa ni usahili ambao
unaendeshwa na wataalam wa maswala ya siasa ili kuwapata wale wenye ubora na
wanaofaa kuwaongoza watanzania
Inasemekana kuwa jimbo
la kikwajini ambalo limeachwa kwa CHADEMA atasimama Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
Zanzibar SALUM MWALIM katika harakati za ubunge.
No comments:
Post a Comment