Wanawake mbalimbali kutoka jumuiya ya wanawake wa chama cha wananchi CUF wakishangilia kwa furaha katika kongamano hilo |
Makamu Mwenyekiti wa
chama cha wananchi CUF mh JUMA HAJI DUNI pamoja na Katibu mkuu wa chama hicho ambaye ni
Makamu wa Rais wa kwanza wa serikali ya Zanzibar Mh maalim Seif Sharif Hamad
Leo wameongoza kongamano Maalumu lililoandaliwa na jumuiya ya wanawake wa chama
hicho iliyokuwa na lengo la kuchangia jumuiya hiyo ili iweze kufanya shughuli
zake za kisiasa nchini.
Kongamano hilo maalum
lililofanyika makao makuu ya CUF Taifa Jijini Dare s salaam lilikuwa na lengo
maalum la kuchangia wanawakle hao wa chama hicho ili waweze kupata rasilimali
za kuwasaidia kuzunguka nchi nzima kutoa elimu kwa wanachama wao hususani
wanawawe wa Tanzania kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kwa sasa.
Burudani katika kongamano hilo |
Akifungua kongamano
hilo mgeni rasmi ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho Mh JUMA DUNI
ALLY amesema kuwa jumuiya ya wanawake ya chama hicho ni kiungo muhimu cha
kuhakikisha kuwa wanawake nchini wanainuka na kuzipigania haki zao hivyo ni
lazima jumuiya hiyo iwezeshwa kwa lengo la kuwasaidia wanawake wote wa Tanzania.
Amesema kuwa kuna mambo
mengi ambayo yanahitaji elimu kwa sasa ikiwemo kuwahamasisha wanawake
kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari ili waweze kupiga kura
katika uchaguzi ujao,kutoa elimu juu ya mauaji ya albino,pamoja na mambo mengi
ambayo yanalikabili Taifa kwa sasa.
Makamu mwenyekiti wa chama hicho JUMA DUNI HAJI akizngumza katika kongamano hilo |
Katika kongamano hili
lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani,wenyeviti na baadhi ya
wabunge wote kwa pamoja wakafanya harambee kwa lengo la kuichangia jumuiya hiyo
ya wanawake wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment