Thursday, May 28, 2015

DC:MTAKA ASEMA ATAKULA SAHANI MOJA NA WAHARIBIFU WA MAZINGIRA WILAYA YA HAI


Mkuu wa Wilaya ya Hai Antony Mtaka akipanda mti katika bonde la mto uwau kata ya Masama Kati Kijiji cha Ng'uni
alipo zindua kampeni ya upandaji miti.

HAI
MKUU wa Wilaya ya Hai  Antony Mtaka amewakemea vikali waharibifua wa mazingira wilayani humo wanao kaidi agizo la kuhifadhi mazingira kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kuhifadhi mazingira.

Mtaka alitoa onyo hilo hapo jana katika Kata ya Masama Kati kijiji cha Ng’uni alipo kuwa katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ambayo nirafiki wa mazingira  katika vyanzo vya maji vya mto Uwau.


Alisema kuwa  suala la utunzaji wa mazingira kwa Mkoa wa Kilimanjaro kwa baadhi ya maeneo  umekuwa ni wakusuasua huku wananchi wakikaidi sheria za utunzaji wa mazingira zilizo tungwa katika maeneo yao.

“Itashangaza  kwa mtu aliye kufa miaka ya nyuma akifufuka saivi nakuuangalia Mlima Kilimanjaro kwa theluji yake ilivyo pungua huku misitu ikiwa imekatwa hovyo na wengine kudirika hadi kulima na kuotesha mazao ndani ya mito na vyanzo vyake”Alisema Mtaka.

Mtaka aliwataka Wenyeviti wa Vijiji katika kata nzima ya Masama Kati  kuwashughulikia wananchi wazembe wanao kaidi sheria za utunzaji wa mazingira katika ngazi husika au ofisini kwake ili waweze kuchukuliwa  adhabu kali na kuwa fundisho kwa wengine kutokana na viongozi kuchoka na tabia hiyo.

“Hawa watu wanao haribu mazingira nataka niwa adhibu kwenye haki na sita muonea mtu aibu ambaye ameshindwa kuyaonea mazingira aibu kwa kuyatunza nita kula nao sahani moja”.Alisema Mtaka.

Akijibu tuhuma zilizopo za wananchi wanao lalamikia kutunza miti kasha kukatazwa  kuitumia pindi inapo kuwa tayari kuvunwa ili kujipatia kipato na kulipa ada ya shule,Mtaka alisema kuwa zitpo taratibu zinazo chukuliwa katika hatua za uvunaji kwa hiyo kinacho takiwa kufanyika ni kuzuia uvunaji holela na pindi mtu anapo taka kuvuna  atatoa taarifa na kuruhusiwa.

“Tuna jua kuwa miti ni sehemu ya biashara hivyo ni lazima ukate mti kisha upande mti,hivyo unatakiwa kuangalia jinsi ya kuvuna mti lakini unatakiwa kuwa uwe umesha otesha miti mingine itakayo kuruhusu kuvuna mti.”Alisema Mtaka

Kwa upande wake Mwenyekiti wa watumia maji bonde la mto pangani Frank Kimaro alisema kuwa zoezi hilo la uoteshaji miti lita kuwa ni la muendelezo ambapo mito yote na mifereji ya watumia maji itatakiwa kupandwa miti rafiki wa mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazaingira unao pelekea uwepo wa uhaba wa maji kwa sasa.
Kwa siku ya jana takribani miti miatano iliwezwa kupandwa katika mto uwau na maeneo mengine ndani ya kata ya Masama Kati.
Zifuatazo ni Picha za upandaji miti katika bonde la mto uwau

Mfanya kazi toka Bonde la mto Pangani PWB akipanda mti

Afisa tarafa kata ya Masama Ndagile Nsajigwa aki andaa shimo kwaajili ya kupanda mti wake
Mjumbe wa watumia maji akipanda miti

Diwani Deogratius Kimaro akijiandaa kupanda mti.
Diwani wa Kata ya Masama Kati Deogratius Kimaro aliye vaa koti akipanda mti wake.

No comments: