Diwani wa kata ya
Ndugubi iliyopo katika Jimbo la Kinondoni mh CHARLES MGONJA leo amekutana na
mabalozi wote waliopo katika kata yake kwa lengo la kuwakutanisha kwa pamoja
kujadili kuhusu kazi ambazo zinafanywa
na diwani huyo pamoja na kuwashukuru madiwani hao kwa kushiriki kikamilifu
katika ujenzi wa mambo ya maendeleo katika kata hiyo.
Akizungumza na mwandishi
wa mtandao huu nje ya mkutano huo amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka
kwa mbalozi hao kuwa wamekuwa hawapati nafasi kama hiyo ya kukutana na kujadili
kwa pamoja na viongozi walio juu yao pamoja na kazi kubwa wanayoifanya,jambo
ambalo limemsukuma kuwakutanisha mabalozi hao kujadili kwa pamoja na kuelewa
kila kitu ambacho serikali yao inakifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Mabalozi mbalimbali waliojitokeza katika kikao hicho |
Amesema kuwa ufanisi wa
kiongozi wa ngazi za juu za serikali hauwezi kuwa na maana kama hauna mahuziano
mazuri na viongozi wa ngazi za chini za wakiwemo mabalozi hao kwani ndio
wanaohakikisha kuwa katika mitaa yote kunakuwa na ulinzi wa kutosha na
kuimarisha amani katika maeneo yote ya kata hizo.
Akizungumza na mabalozi
hao diwani MGONJA ameanisha mambo mbalimbali ambayo serikali yake imefanya
katika kata hiyo kama ujenzi wa maabara katika shule za secondary ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK KIKWETE,
huku changamoto ikibaki kuwa upatikanaji wa vifaa katika maabara hizo,ujenzi wa
barabara katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo pamoja na maendeleo makubwa
katika secta ya afya na maji.
Akizungumzia joto la
uchaguzi ambalo limeanza kupanda kwa kasi ndani ya chama cha mapinduzi amesema
kuwa ni nafasi sasa ya wanachama wa chama cha mapinduzi katika kata hiyo
kutumia nafasi yao ya kidemocrasia ya kutangaza nia na baadae kugombea katika
nafasi mbali mbali za uongozi katika kata hiyo na jimbo kwa ujumla lengo likiwa
ni kukisaidia chama hicho kupata viti vingi zaidi vya udiwani na ubunge katika
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo baadae mwaka huu.
No comments:
Post a Comment