WATU
WATANO WATHIBITISHWA KUFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM KUTOKANA NA MAFURIKO
Watu
watano wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za
mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Mvua hizo zinazonyesha kwa
siku tatu mfululizo zimesababisha vifo vya watanzania hawa katika maeneo
tofauti ya jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:
1.
Mnamo tarehe 06/05/2015 majira ya saa
moja kamili usiku huko maeneo ya Magomeni Kinondoni jijini Dar es Salaam mtu
mmoja jina SHABAN S/O IDD, Miaka 73, Mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto
ng’ombe alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo. Mwili wake ulipatikana siku
iliyofuata 07/05/2015 akiwatayari amekwishafariki dunia na umehifadhiwa katika
hospitali ya Mwananyamala.
2.
Kifo kingine kilitokea tarehe
07/05/2015majira ya saa sita kamili
mchana huko maeneo ya Mwananyamala Mbuyuni Kata ya Mwananyamala, OysterBay,
Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja aitwaye MASUMBUKO S/O DOUGLASS
@ LIMAMU, Miaka kati ya 50-55, mkazi
wa Mwananyamala Mbuyuni, alianguka na kufariki dunia ghafla wakati anatoa maji
yaliyoingia nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa
na tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akihangaika kutoa maji, ugonjwa huo
ulimpata na kuanguka kwenye maji na kufariki dunia baada ya kukosa msaada wa
haraka. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.
3.
Mtu
mwingine mwanaume RASHIDI S/O HASSAN, Miaka 36, Mkazi wa maeneo ya Mvuruhani
Pemba Mnazi Kigamboni jijini Dar es Salaam alizama katika mkondo wa maji
unaoelekea baharini tarehe 06/05/2015. Mwili wake ulipatikana tarehe 07/05/2015
ukiwa unaelea majini umbali wa mita 500 toka eneo alilozama.
4.
Kifo
kingine kimetokea tarehe 06/05/2015 huko Yombo Makangarawe ambapo mtoto aitwaye
GLORIA D/O MREMA, mwaka mmoja na miezi mitatu alipotea baada ya watoto wenzake
kumuacha wakati wakicheza pamoja. Juhudi za kumtafuta zilifanyika bila mafanikio
hadi mwili wake ulipopatikana ukiwa unaelea majini katima mto mzinga akiwa
tayari ameshapoteza maisha. Mwili
umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke
5.
Kifo
kingine kimetokea tarehe 08/05/2015 saa moja kamili asubuhi huko maeneo ya
Kinondoni Mkwajuni, Kata ya Mkwajuni Wilaya ya Kinondoni ambapo mtu mmoja
mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri
kati ya miaka (40-45) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, alikutwa amefariki dunia.
Mwili umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi.
Pamoja
na vifo hivyo kuripotiwa, pia mtu mmoja ajulikanae kwa jina la MABULA S/O
MOSSES, Miaka 65, Mkulima, Mkazi wa Vingunguti,
Buguruni wilaya Ilala amevunjika mguu wake wa kulia sehemu ya chini ya
goti baada ya kuangukiwa na ukuta wa Godown la FIDA S/O HUSSEIN lililopakana na
nyumba yake. Pia ukuta huo umesababisha uharibifu wa vitu mbalimbali. Majeruhi
amepekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu.
Katika
kata ya Mchikichini, taarifa ya mafuriko inaonyesha takribani nyumba 60 hadi 70
zimefunikwa na maji hadi juu ya mapaa ambapo wakazi wake tayari walikuwa
wamehama kufuatia agizo la Serikali kuwa wahame maeneo hayo. Pia takribani watu
30 hadi 35 wamejihifadhi katika shule ya Srkondari Mchikichini.
Katika
Kata ya Jangwani, zipo nyumba zinazokadiriwa kufikia 90-100 zimefunikwa na maji
hadi juu ya paa. Wakazi takribani 250-300 walihama mapema kufuatia taarifa hiyo
ya Serikali. Aidha watu wanaokadiriwa kati ya 25-30 nao wamejihifadhi katika
Shule ya Sekondari Mchikichini.
Aidha,
maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ni Keko, Chang’ombe
maduka mawili, Yombo Vituka, Vingunguti, Africana, Msasani Bonde la Mpunga,
Eneo la Jangwani, Manzese, Kigogo, Mburahati, Boko Basihaya, na maeneo mengine
ambayo taarifa zake bado hazijapokelewa
Barabara
zinazounganisha katikati ya Jiji na pembezoni zimeharibika na hivyo kusababisha
kutolewa maelekezo barabara hizo kufungwa ili kupunguza madhara ambayo
yangeweza kutokea.
Aidha,
madaraja mbalimbali yameharibika hivyo kukata mawasiliano kutoka upande mmoja
kwenda upande mwingine. Kwa mfano daraja la linalounganisha Mbagala na Mtoni
Kijichi maarufu kama njia ya ng’ombe. Daraja lingine ni lile la Kinyerezi
ambalo halipitiki baada ya kusombwa na maji.
Jeshi
la Polisi kwa kushirikiana na Serikali limejiandaa kwa hali ya dharura
itakayojitokeza. Pia Jeshi la Polisi limejipanga kukabili foleni kwa kuhusisha
askari wa vikosi mbalimbali ili kukwamua tatizo hilo ambalo limesababishwa na
uharibifu wa miundombinu.
Aidha
nawataka wananchi wote kuchukua tahadhari ya hali ya juu hasa wale waishio
maeneo ambayo ni mikondo ya maji au watumiaji barabara zinazopitiwa na mikondo
hiyo. Wananchi wanaombwa kutoa taarifa za mapema na haraka pindi wanapoona au
kugundua kuna maeneo au jambo
linalohatarisha maisha yao na ya watu wengine.
NB:
Wakati huo huo zimepokelewa taarifa za kupatikana kwa miili ya watu watatu
waliofariki ambayo inafanyiwa uchunguzi katika hospitali mbalimbali jiji Dar es
Salaam ili kujua kama vifo hivyo vimetokana na mafuriko yaliyosababishwa na
mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Taarifa kamili zitatolewa kuhusu wajihi wa
watu hao na wako katika hospitali gani
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment