LICHA ya wadau mbali mbali wakiwemo wadau wa Mambo ya Habari,wanasiasa pamoja na wanaharakati kumtaka Rais Jakaya Kikwete asiusaini Mswaada wa Uharifu wa Mitandao nchini wa Mwaka 2015-
Hatimaye ni kama Rais Kikwete amepuuza kilio hicho na kusiani Mswaada huo na kuwa Sheria Rasmi na kuanzia kutumika kuanzia kesho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akithibitisha kusainiwa kwa Mswaada huo na kuwa sheria Rasmi na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa leo jijini Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema Baada ya Mswaada huo kupitia sehemu mbali mbalina kuonekana hauna Tatizo lolote ndio ukamfanya Rais Kikwete kusiani Mswaada huo.
Waziri Mbarawa amesema Sheria hiyo itasaidia kupunguza Makosa mbali mbali ya watu wanaofanya kwa Makusudi kwenye Mtandao Jambo ambalo anadai italiweka Taifa salama na kuondokana na Tabia iliyojijengeka kwa Baadhi ya watu kuandika Habari na kusambaza Taarifa za upotoshaji kwenye Mitandao ya Kijamii.
Pamoja na hayo Waziri Mbarawa amesema kwa sasa baada ya Rais Kikwete kusaini hatua inayofuata ni kazi ya Wizara hiyo kuwaelimishwa wananchi kuijua sheria hiyo ili kuanza kutimika Rasmi.
Aidha,Waziri huyo amesema kwa wale wadau mbali mbali wa Masuala ya Habari na wanasiasa pamoja na Wanaharakati ambao walikuwa wanaubeza Mswaada huo,wanatakiwa kuwasilisha hoja zao kwenye Wizara yake ili hatua zichukuliwe kwenye Vipengele ambavyo Wizara hiyo itaviona labda vitakuwa na Utata .
Vilevile akawataka Watanzania kuipokea sheria hiyo kwa Manufaa makubwa kutokana na Uharifu wa Mitandao hivi sasa ambao ulikuwa unawasumbua.
Kusaniniwa kwa Msaada kunatafsiliwa na wadau mbali mbali wa Masuala ya Habari nchini ni kama umeendelea kunyonga Uhuru wa Habari nchini kutokana na Sheria hiyo kuwepo na Vifungu Kandamizi kwa watu wanaotoa Taarifa kwa Umma kwa njia ya Mitandao.
Wadau mbali mbali wa masuala ya Habari waliokutana tarehe 2 ya mwezi huu Mkoani Morogoro siku ya Vyombo Vya Habari Duniani walimtaka Rais Kikwete kutosaini Mswaada huo kwani utaiweka Njia panda Taifa na wakadai Uhuru wa Habari unazidi wambwa Msalabani kutokana na Vipengele vilivyopo kwenye Sheria hiyo mpya.
Wanasheria wananena
Wanasheria Mmoja Maarufu hapa Jijini aliyezungumza na Mtandao huu amesema kitendo cha Rais kikwete kusaini Mswaada huo na kuwa sheria ni kama kuua Rasmi Uhuru wa kutoa habari na kupata Habari.
“kusema kweli Rais Kikwete amenisikitisha sana kusaini Mswaada wenye utata leo Rais Kikwete wakati anaingia madarakani alitoa uhuru mkubwa wa kujieleza na kutoa maoni inakuwaje sasa anakubali kusaini mswaada wenye utata kama huu ambao unamkosa chungu mzima”amesema Mwanasheria.
Gwaji huyo wa Sheria alizidi kuongea kwa Uchungu amesema kwa sasa Jinsi hali anavyoiona basi watanzania wengi wajiadhali kuishia magerezani kutokana na kuwa na Vipengele anavyodai vina utata.
No comments:
Post a Comment