Thursday, May 7, 2015

MADIWANI TEMEKE WALIA NA MFUKO MAALUM WA MAAFA MBALIMBALI

 Na Mwandishi wetu.
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Temeke wamuomba Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha ana boresha

mfuko maalumu wa Mahafa ili kuweza kukabiliana na majanga mbali mbali
yanayojitokeza badala ya kutegemea ofisi ya Waziri mkuu.

Hayo yalisemwa ,na Diwani wa Kata ya Kurasini Wilfred Kimati wakati

alipokuwa akitoa hoja katika Baraza la Madiwani ya Halmashauri hiyo.
Akizungumza na Madiwani,Watendaji,na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo,diwani huyo alisema wananchi wanakumbwa na mahafa makubwa yakiwemo ya Mvua kubwa ambazo zinaendelea kunyesha sasa na kusababisha mafuriko

hali inayopelekea jamii kupoteza makazi yao hivyo Halmashauri inatakiwa kutenga bajeti ambayo itaweza kupoza machungu
ya wananchi kuliko kuendelea kutegemea mfuko wa dharura wa ofisi ya Waziri Mkuu.


Alisema kuwa kwakuwa Halmashauri ina vyanzo vingi vya kujikusanyia mapato yake ya ndani lakini bado Halmashauri
haina mfuko wake maalumu ya kukabiliana na Mahafa ya kuweza kukabiliana na Maafa makubwa yanayowakumba wananchi wake.

"Licha ya kuwepo kwa Mfuko wa Maafa ambao upo chini ya Waziri Mkuu,lakini  pia bado kuna haja ya kuwa na Mfuko 

wetu maalumu wa Mahafa kwaajili ya kukabiliana hali za hatari zinazo wakumba wananchi,na uwezo wa fedha upo natoa rai tulitatue
hilo"alisema.

Naye Naibu Meya wa jiji  la Dar es salaam ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tandika,Zena Mgaya amekiri kuwa mitaro nayo imengia sana uharibifu wa miondombinu kutokana na kushindwa kutililisha maji vizuri.

No comments: