Kituo cha sheria na
haki za binadamu(LHRC) kimezindua report yake ya haki za binadamu ya mwaka 2014
uzinduzi ulioenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya uangalizi na utetezi wa haki za
binadamu wa kituo hicho huku wakijivunia miaka 20 yenye mafanikio makubwa
katika kueneza haki za binadamu Tanzania.
Akizindua taarifa ya
haki za binadamu ya mwaka 2014 hii leo Jijini Dar es salaam Jaji mstaafu na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa tume ya haki
za binadamu Jaji Amir Manento amesema lengo kuu la kuzindua Taarifa hii ni kujenga
uelewa juu ya maswala ya kisheria na Haki za Binadamu na kutoa ushawishi wa
kuboresha katiba,kutetea na kuheshimu haki za binadamu nchini.
Amesema kuwa ni
mafanikio makubwa ya kujivunia kwa kituo cha sheria na haki za binadamu
kufikisha miaka 20 ya utumishi ambao wameonekana wazi kuwa wamewasaidia
watanzania wengi katika maswala ya kisheria na haki za binadamu jambo ambalo
amesema kuwa ni lazima wapongezwe kwani kazi waliyofanya ni kubwa.
Amengeza kuwa kituo
hichi kimekuwa mstari wa mbele katika kufungua kesi mbalimbali ambazo zina
maslahi kwa umma ili kushinikiza uwajibikaji,mabadiliko ya sera na pia ulinzi
wa haki za binadamu ambapo amesema kuwa ni udhubutu aina yake kufanya hivyo.
Ametaja mashauri ambayo
yamewahi kufunguliwa na kituo hicho na kuwasaidia watanzania ni pamoja na
shauri dhidi nya waziri mkuu Mh MIZENGO PINDA,shauri la takrima,shauri la
kupinga uanzishwaji wa mfuko wa jimbo,shauri la kutaka ulinzi wa kutaka ulinzi
wa watu wenye ulemavu wa ngozi na mashauri mengine mengi ambayo yalikuwa na
maslahi kwa umma.
Kwa upande wake Mkurungenzi wa kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu Dr Hellen kijo Bisimba amesema kituo cha sheria na haki za Binadamu
kimetoa ushauri kwa serikali na wadau mbalimbali kufanyia kazi mapendekezo
yaliyotolewa katika Taarifa
iliyozinduliwa leo ilikuboresha hali ya haki za binadamu nchini na kuongeza kuwa ukiukwaji wa sheria na haki Za binadamu unatokea kwa sababu ya ukosefu wa elimu.
Amesema kuwa katika Report
hiyo imeonyesha maswala kadhaa ambayo bado yamekuwa matatizo makubwa Tanzania yakiwemo
maswala ya uwajibikaji wa viongozi pindi wanapokumbwa na kashfa za
ufisadi,swala la kuvamiwa na kupigwa kwa askari nchini Tanzania,pamoja na
maswala ya haki za makundi mbalimbali wakiwemo watoto na wakina mama.
Aidha katika taarifa
hiyo iliyozinduliwa leo imeangalia
maeneo mbalimbali toka mwaka 2002 hadi kufikia mwaka 2014 .kituo cha sheria na haki za binadamu kimetoa
mapendekezo mbalimbali kwa serikali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya haki za
binadamu katika ngazi zote za elimu na na serikali, serikali ichukue hatua za haraka kwa wavunjaji wa
sheria na haki za binadamu ili iwe fundisho kwa jamii inayotuzunguka.
No comments:
Post a Comment