Wednesday, May 27, 2015

MWENGE WA UHURU WAWASILI DAR ES SALAAM

 Na Isaac Magesa
MWENGE wa uhuru umewasili rasmi jijini Dar es salaam ukitokea  mkoani Kaskazini Pemba ili kuzindua miradi 19  ya maendeleo ya jamii yenye thamani ya sh bil 31 zilizotokana na mapato ya ndani.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es salaam,Jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Said Mecky Sadiki alisema kuwa Mwenge huo utazindua miradi 19 ndani ya Mkoa wake ambayo inagharimu zaidi ya bil 31.

Alisema kuwa kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu ni uandikishaji katika daftari ya kudumu ni haki ya msingi ya kila mwananchi hivyo wananchi wanatakiwa kujitokeza kujiandikisha.

No comments: