Sunday, May 24, 2015

PICHA 20--TIZAMA MBOWE,GWAJIMA,PROFESA J,FLORA MBASHA,NA CHADEMA WALIVYOITIKISA TANZANIA LEO


Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo chadema mh FREMAN MBOWE akizindua kikosi maalimu cha ulinzi katika jimbo la kawe maarufu kama RED BRIGDED ambao wamekuwa na kazi ya kulinda usalama wa viongozi wa chama chao.
 Mwenyekiti wa chama cha chadema FREMAN MBOWE amesema kuwa endapo sheria ya kuvitaka vyombo vyote vya habari Tanzania kuonyesha Taarifa ya Habari moja kutoka shirika la utangazaji TBC itafikishwa bungeni basi bunge hilo halitamalizika na badala yake wataamua kufanya fujo za maksudi kwani sheria hiyo ni sheria ya kuuwa kabisa uhuru wa mtanzania kupata habari.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa kawe waliojitokeza katika mkutano wa hadhara muda huu Jijini Dar es salaam Amesema kuwa kuna sheria ambayo chama cha mapinduzi kimejipanga kuifikisha katika bunge ambayo inazitaka stesheni zote za tv na redio kujiunga na TBC kwa ajili ya kupata taarifa ya habari,sheria ambayo amesema kuwa ni muendelezo wa kuwabana watanzania baada ya ile sheria ya mtandao kupitishwa kinyemela.
Swala la BVR

Mwenyekiti huyo amesema kuwa anamtaka mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza siiku za kuandikishwa daftari hilo kwani siku saba zilizowekwa katika kujiandikisha hazitoshi na ni mpango wa kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanakosa fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka wenyewe.

Mbowe ameongeza kuwa hakuna ubishi kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imechoka na ni lazima mwenzi wa kumi wafanye maamuzi ya kuiondoa madarakani kwa lengo la kupata serikali nyingine ambayo inaweza kusikiliza shida zao



Picha zikimuonyesha mwenyekiti mbowe akizindua kitabu maalum cha HALIMA MDEE ambacho kinaelezea mafanikio ya mbunge huyo katika jimbo lake

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili flora mbasha akitumbuiza pamoja na waceza shoo wake



FLORA MBASHA akitumbuiza nyimbo yake mpya aliyotunga kwa ajili ya kumpongeza mbunge halima mdee kwa kazi kubwa aliyofanya.




Askofu gwajima akiwasili katika viwanja hivyo


Viongozi wa kikosi cha ulinzi kawe wakitoa heshima kwa kamanda mbowe kabla ya kukagua gwaride hilo




Msanii profesa J akiwasha moto kwenye jukwaa ambapo aliwarusha mashabiki wake kwa nyimbo mbalimbali za muziki wa kizazi kipya

Wingi wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo

No comments: