Rais wa msumbiji Mh. Filepe Jacinto Nyussi leo amelihutubia bunge la jamhuri ya Muugano wa Tanzania na kusisitiza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na msumbiji tangu enzi za harakati za kutafuta uhuru wa msumbiji ambapo tanzania iliikuwa msaada mkubwa kwa nchi hiyo.
Rais Nyussi aliyeambatana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete amesema msumbiji itaendelea kuimarisha zaidi uhusiano wa kijamii, kiuchumi na kiusalama baina ya msumbiji na tanzania kuelezea dhamira yake ya kulihutibia bunge la tanzania siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
Katika hotuba yake Rais Nyusi amesema serikali yake imejitolea kuimarisha uhusiano wa miaka mingi kati yake na Tanzania na hivyo angependa kuwaalika wawakilishi wa bunge la Tanzania nchini msumbiji kusudi kuweza kujifunza mambo mbali mbali.Kwa upande wake Spika wa bunge nchini Anne Makinda amempongeza rais
Nyusi kuchaguliwa na watu wa Msumbiji kuwaongoza na hivyo kuchukua uamuzi wakuja nchini kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe na hivyo kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwaniaba ya wabunge wote Spika Makinda amemshukuru Rais Nyusi na kusema kuwa tangu ya uongozi wa waasisi wa mataifa haya,wamechukua hatua madhubuti za kukuza uhusiano, na ziara yake hapa nchini ni kielelezo tosha kuwa mabunge ya nchi zetu mbili yamekuwa na uhusiano wa muda mrefu, kupitia vyama vya mabunge na wamekuwa wakishiriki katika semina na ziara mbalimbali za mafunzo,hivyo wanaendelea kukuza uhusiano huu.
Makinda amesema ujio wa Raisi Nyusi imekuwa na faraja nzuri kwa taifa hivyo watampa zawadi ya picha ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati wa picha ya pamoja.
|
No comments:
Post a Comment