Wa kwanza kushoto August Temu Mwenyekiti wa Red Cross Kilimanjaro,katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Hai Zuhura Chikira na Mkurugenzi Wilaya ya Hai Said Ahmed Said Mderu wakipokea msaada kwa waathirika wa mafuriko. HAI
MKURUGENZI Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Hai Said Ahmed Said Mderu amewataka wahanga wa
mafuriko wa kata ya Rundugai na Weruweru wanaopokea misaada
mbalimbali kuitunza na kuitumia ili kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu.
Ameyasema hayo leo
alipokuwa anapokea misaada mbalimbali kutoka shirika la Msalaba Mwekundu
Kilimanjaro katika kijiji cha Kawaya Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Mderu amesema
kuwa ikiwa wahanga hao wa mafuriko watakuwa wanatumia misaada wanayo
pelekewa pasipo utaratibu maalumu utasababisha mashirika mengine pamoja na
wadau mbalimbali kusitisha kupeleka hudumu muhimu maeneo hayo ,hivyo ni vema
waka onesha hali ya ustaarabu katika kutumia misaada
hiyo.
"itashangaza sana
kwa vyandarua vinavyo tolewa kutumika katika kuvulia samaki au kufugia
kuku kama watu wengine wanavyo fanya niwaombeni msifanye hivyo."Alisema
Mderu.
Pia amepongeza wadau
mbaimbali ambao ni benki ya NMB pamoja na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kwa
misaada waliyo toa katika kaya zilizo kumbwa na mafuriko jambo ambalo limewapa
matumaini makubwa wananchi hao.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kilimanjaro August Temu
ameserma kuwa watazidi kutoa huduma na misaada mbalimbali kwa wananchi wanao
kutwa na majanga mbalimbali ili kuweza kuonesha upendo baina ya shirika na
wananchi kwani ni jukumu la shirika hilo kutoa misaada kama hiyo.
Amesema kuwa
mbali na wananchi kutegemea mashirika na wadau mbalimbali bado kuna nafasi
kubwa ya wananchi wenyewe kupendana na kusaidiana katika majanga ili kuweza
kuonesha uzalendo huku akiwataka wananchi kutoa misaada kama vile
mavazi,vyakula na malazi kwa waathirika wa mafuriko hayo.
"Tusipende kila
kitu tusaidiwe kutoka nje ya nchi sisi wenyewe tunaweza tukasaidiana kutatua
matatizo yetu pasipo kutegemea nje ya nchi hivyo naombeni tuwe na utamaduni wa
kusaidiana sisi kwa sisi".Alisema Temu.
Shirika hilo la
Msalaba mwekundu limetoa misaada kwa wanakaya wote wa kata ya rundugai na
weruweru walio kumbwa na mafuriko hayo ikiwa ni pamoja na mablanketi
125,vyandarua 100,mabeseni 120,ndoo 200 na dawa za kusafisha maji katoni 20.
Tazama picha za upokeaji
wa msaada huo kwa waathirika wa mafuriko.
|
No comments:
Post a Comment