Tamko
la Mhe.Nyalandu kuhusu shutuma za Mbunge Mhe.Nassari
“Nimesikitishwa sana na
kauli ya Mhe. Joshua Nassari ambayo ameongea kwa kudhalilisha
utendaji wangu serikalini.
Naomba Mh.Nassari
afahamu kuwa kunikashifu pasipo kueleza masuala ya kisera au ya kiutendaji ni kupungukiwa na busara ya kawaida
kwa kiongozi aliyepaswa kuwa wakilisha wapiga kura wake kwa hoja. Itakumbukwa kuwa
hivi karibuni Mhe.Nassari aliniita Jimboni kwake Arumeru Mashariki akiniomba nitatue
tatizo lililohusu wananchi wa jimboni kwake waliokuwa wanahitaji matibabu katika
hospitali ambayo ilikuwa sharti upitie ndani
ya hifadhi iliufike kutibiwa.
Nilikwenda kuwaona wagonjwa
na kuitembelea hospitali hiyo na kulitatua tatizo hilo siku hiyo hiyo. Kwangu kama Waziri, haliku wasuala la kufanyia
siasa afya za Watanzania, pamoja na yeye kuwa Mbunge wa upinzani.
Nilimheshimu na kukubali
wito wake kwaniabaya wananchi.
Nimewatembelea na kuwatia moyo maaskari wetu nchi nzima na kuwapelekea vitendeakazi.
Nimefurahi pamoja nao na
kulia pamoja nao. Nimeenda kuwafariji familia zawapiganaji wetu waliopoteza maisha
kwa kuuawa wakilinda raslimaliza Taifa, watu ambao Mhe.Nassari anawabeza.Tumepambana
naujangili na tunaendelea kuushinda. Tumeleta magari, silaha, ndege, helicopters, na raslimali nyingi ilikulinda
raslimali za Taifa. Busara haisomewi ilani kumshukuru Mungu akusaidie kujua
matumizi ya ulimi. Nimesikitishwa sana na kauli za uongo na kuzusha za Mhe.Nassari.
Imeandikwa, usimsingizie
jirani ya kouongo.”
Mh.
LazaroNyalandu.
No comments:
Post a Comment