Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mohamed Raza akionesha baadhi ya vifungu vya sheria vilivyopo kwenye kitabu kidogo cha sheria za Zanzibar,Mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa BB Swahili nchini Tanzania,Arnold Kayanda akifanya mahojiano mafupi na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo-Globu ya Jamii
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mohamed Raza amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kutafuta mgombea wa nafasi ya urais mwenye sifa na sio watu wanaotoa fedha kwa ajili ya kutaka kupendekezwa katika kiti hicho.
Raza ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema fedha nyingi zinamwagwa Zanzibar kwa ajili ya watu wanaotaka Urais na fedha hizo zinatoka kwa wafanyabiashara ambao watataka zirudi au kumwamulia Rais katika nafasi za uteuzi wa baraza la mawaziri ambao watanufaika katika kuhakikisha mambo yao yanakwenda.
Amesema vyombo vya dola visaidie katika kupata rais mwenye sifa kwani ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Ulinzi na Usalama, na bila kufanya hivyo watakaoumia ni watanzania huku viongozi wakijinufaisha wenyewe.
Raza amesema kuwa CCM ikifanya vibaya katika kuchagua mtu sahihi, kuna upande wa pili wa UKAWA wana nguvu kutokana na mambo yanayoendelea nchini kutokwenda sawa na wanatumia hoja na hawawezi kuzuilika hata wamwagiwe maji ya pili pili wakitaka kufanya maandamano.
Raza ambaye ni Mbunge Muwakilishi wa Jimbo la Uzini amesema kuwa hali inayokwenda sasa sio nzuri kutokana na bajeti ya Zanzibar kukosa wafadhili kutokana na watu waliojipatia fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow wakati wazanzibar hawajahusika kujipatia fedha hizo.
Amesema kutokana na kukwama kwa wafadhili, wanaoathirika ni wananchi kwani posho ya mbunge ya siku ndio fedha ya mwananchi ya mwezi mmoja hivyo kutokana na dola kushuka wataathirika kwa kiwango kikubwa.
"Aidha kutokana mambo yanayoendelea tunahitaji kuwa na viongozi ambao wanaangalia wananchi na sio wale ambao wanajiangalia wenyewe kwa masilahi yao binafsi huku wanaowagua wakiwa na hali mbaya",alisema Raza.(Muro)
No comments:
Post a Comment