Sunday, May 31, 2015

TIZAMA ALICHOKIFANYA TENA DK SLAA ZIARA YAKE


Katibu Mkuu Dk. Slaa yuko katika ziara ya kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura linavyokwenda na kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu; ambapo pia anakagua maandalizi ya chama kwenda kushinda uchaguzi kwa kushirikiana na vyama washirika wa UKAWAHapa ni Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma ambapo Dkt. Slaa amehutubia mkutano mkubwa wa kihistoria kuwahi kufanyika mjini hapo.
 

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mwandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Mailosy Bukuku namna mashine ya BVR zinavyofanya kazi katika kituo cha Igamba Wilayani Mbozi, Mbeya jana. 


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa , akizungumza na wananchi waliojikeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga katika kijiji cha Igamba wilayani Mbozi jana. 


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mwandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Eldah Chakachaja namna mashine ya BVR zinavyofanya kazi katika kituo cha Igamba Wilayani Mbozi, Mbeya jana wakati Dk Slaa alipfanya ziara ya kutembelea vituo vya kujiandikia wananchi wilayani Mbozi Mbeya. 




No comments: