Imeelezwa kuwa vitendo
vya ugaidi na mauaji yanayofanywa na watu mbalimbali barani Africa na duniani kwa ujumla hayahusiani hata
kidogo na dini ya kiislam kama ilivyokua ikielezwa na wadau mbalimbali kuwa
mauaji hayo yanahusiana na imani ya dini ya kiislam.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dare es salaam na kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA
ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA wakati akizungumza katika kikao cha
pamoja cha viongozi wa dini zote kikao kilichoandaliwa na chuo cha kidini cha
IMAM JAFAR SWADIQ,kigogo Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa ugaidi
katika bara la Africa umekuwa ukitafsiriwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa katika
msukumo wa dini ya kiislam jambo ambalo amesema kuwa watanzania wanapaswa
kuelewa sio sahihi kuwatuhumu waislam kwa ugaidi kwani hakuna kitabu chochote
kinachoruhusu muislam kufanya mauaji kwa mwadamu mwenzake.
Amefafanua kuwa
mivutano na Ugaidi uliyopo barani Africa umekuwa ukisababishwa na mambo matatu
ambayo ameyataja kuwa ni ugaidi wa kifikra,kiuwezo na ugaidi wa kudai haki.
Wajumbe mbalimbali wakichangia |
Aidha Ameongeza kuwa
dini zote duniani hakuna hata ushaidi wa dini moja ambayo inaruhusu ama
kushabikia vitendo vya mauaji ya kigaidi yoyote yanayotokea afrika..
Katika hatua nyingine
sheikh JALALA akizungumzia swala ambalo limekuwa likitamkwa na serikali kuwa
viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakiwafundisha vijana wao wa mbinu na njia
za ugaidi ameitaka serikali kuacha kauli hizo kwani ni kauli za kichochezo na
zisizo na ushahidi wowote na badala yake wafwatilie swala hilo kiundani pasipo
kuitaja dini yoyote kuhusika.
Akizungumza katika
kikao hicho muwakilishi wa wakiristo katika mkutano huo pastor PRINCE ERASTO
IKONGO kutoka pentecoste Tabata amesema kuwa viongozi wa dini za kikiristo
wamekuwa na hofu kubwa juu ya ndugu zao ambao ni waislam hofu ambayo
wamejengewa kuwa viongozi wa dini za kiislam pamoja na waumini wao ni watu wa
mauaji na ugaidi jambo ambalo amewatoa wasi wasi wakristo na kuwataka kujenga
umoja na mshikamano juu ya waislam na dini zote Tanzania ili kuidumisha amani
ya nchi.
Amesema kuwa hofu
iliyojaa miongoni mwa viongozi wa dini za kikristo ni hofu ambayo imejengwa na
wanadamu kuwa waislam ndio wanaohusika na mauaji mbalimbali ambayo yanatokea
duniani ya kigaidi jambo ambalo linapaswa kufutika miongoni mwa wakristo ili
waweze kudumisha umoja wanchi.
Kikao hicho kimefanyika
leo Jijini Dar es salaam Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya ukombozi
wa bara la Africa kilikua na kauli mbiu ya TUUNGANE KWA PAMOJA KUUPINGA UGAIDI
AFRICA ambapo kimehudhuriwa na viongozi kutoka dini zote huku lengo kuu la
kikao hicho likiwa ni kujadili kwa pamoja maswala ya ugaidi barani Africa na
kuona ni njia gani zinazoweza kutumika kuondokana na tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment