Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi akiaga mwili wa Marehemu Edson Kamukara |
KAULI aliyeitoa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dokta Reginald Mengi wakati wa Kumuaga Mhariri wa Gazeti la Mawio pamoja na Mtadandao wa Mwanahalisi Oline Marehemu Edson Kamukara,Mapya yazidi kuibuka ambayo yamefichika.(Mtandao huu umedokezwa),Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli hiyo ya Dokta Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT) aliitoa Jumamosi ya wiki iliyopita kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati wa kuaga mwili wa Edson Kamukara,
Kwa mujibu wa Dokta Mengi alisema waandishi wa Habari nchini wanaficha ukweli juu ya kueleza sababu ya kifo cha marehemu Kamukara.
“Mimi sitaki kutafuna maneno. Kamukara amekufa wakati akifuatilia habari moja kubwa. Katika siku za hivi karibuni, alikataa mamilioni ya pesa ambayo aliahidiwa kama angeacha kuchunguza kuandika habari hiyo, lakini yeye alikataa kupokea pesa hizo na akaandika habari na kuitoa.”alisema Dokta Mengi
Kwa mujibu wa Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata kutoka ndani ya Gazeti la Mawio zinasema Habari ambayo alikuwa anailenga Dokta Mengi ni ile iliyotoka kwenye chapisho la Gazeti la Mawio la Tarehe 18 mwezi huu na ilikuwa inazungumzia ufisadi wa Kampuni mpya ya simu inayohusika zaidi ya masuala ya (internet) ya 4G mobile .
Kwa mujibu wa Chanzo chetu hicho kinasema Habari hiyo iliibua mbinu chafu zinazokwenda kinyume na sheria ya Usajili wa Makampuni,na ulikuwa unafanywa na wanasiasa mbali mbali.
Wanasiasa hao ambao ni Mbunge wa Wawi (CUF), kisiwani Zanzibar, Hamad Rashid pamoja na Kigogo wa chama cha Mapinduzi CCM Nazir Karamagi ambapo kwa mujibu wa Habari hiyo ya kiuchunguzi iliwaonesha wanasiasa hao wakifanya udanganyifu ikiwemo kupora hiza za watu waliokuwa wamewekeza kwenye Kampuni hiyo.
“Sisi tunajua Habari hiyo anayoisema Dokta Mengi ni ile ya Ufisadi kwenye kampuni ya 4g mobile ambayo Marehemu Kamkukara alipokuwa anaifuatilia aliambiwa achane nayo atapewa mamilioni ya Pesa ila marehemu Kamukara ni miongoni mwa waandishi wachache wenye misimamo akaikataa pesa hiyo na akaitoa habari yenyewe,kama ulivyoiyona”
Mtoa taarifa wetu huyo wa Gazeti la Mawio ameongeza kwa kusema kuwa “Ujue Habari ilikuwa na Mwendelezo,sema Gazeti la Mawio la Alhamisi ya tarehe 27 aikuendelea kutokana marehemu kamukara kutokuwa Ofisi,ndio maana aikutoka ila nakuhakishishia Gazeti letu ni makini na ile habari tuitaichapisha maana alikuwa ameshaimaliza kuifanyia uchunguzi,na utaiyona wiki hii”
Marehemu Kamukara ambaye amezikwa jana nyumbani kwao katika kijiji cha Ihangiro, Muleba Kusini, mkoani Kagera, alifikwa na mauti Juni 26, 2015 saa 12:30 jioni nyumbani kwake, Mabibo jijini Dar es Salaam,.
Sababu ya kifo chake ambapo Taarifa zinawanukuu majirani wakisema, Kamukara alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa, ghafla alianguka ambapo majirani walimsaidia kumpepea na baadae kumpeleka kwake ambako alipumzika hadi alipopata nguvu.
Hata hivyo, ghafla majirani walianza kusikia kishindo ndani ya nyumba hiyo na baada ya kuingia ndani, walimkuta akiwa ameanguka, huku fulana aliyokuwa amevaa ikiwa imeungua moto na yeye kutoka damu nzito iliyotapakaa kwenye sakafu.
Aidha, televisheni ilikuwa imepasuka, pamoja na vifaa vingine vidogo vidogo vya ndani navyo vilikutwa vimepasuka, jambo ambalo linaonyesha kama kulikuwa na purukushani au alikuwa akivunja vitu hivyo.
No comments:
Post a Comment